Tuesday, June 5, 2012

Nicki Minaj vs Hot 97: Sitaki kuombwa msamaha - Nicki


Baada ya maDj wa radio maarufu ya Hot 97 ya New York, Marekani, Funkmaster Flex na Peter Rosenberg kumdhalilisha Nicki Minaj ‘live onstage’ kwenye concert ya Summer Jam jumapili iliyopita, amesema haitaji kuombwa msamaha.

Nicki alilazimika kutofanya show kutokana na amri kutoka kwa bosi wa YMCMB  Lil Wayne, baada ya dj wa Hot 97 DJ Peter Rosenburg kuiponda single yake ya Starships iliyopo kwenye albam yake ya pili ya Pink Friday: Roman Reloaded kama 'bullshit' wakati wa PA.

Funk Flex aliwashambulia Young Money stejini kwa kusema, “I'm dedicated to tearing you down!"

"We aint f**king with commercial rappers no more!," Flex aliongea wakati akicheza wimbo wa Rihanna Birthday Cake. "If you lost the f**king streets, it's your fault!"

Dj huyo mkongwe aliendelea kwa kuponda mauzo ya Pink Friday: Roman Reloaded, kwa kuongeza, “if you don't go gold, it's your fault! We gon' show you mama! You think you didn't sell any records this time?"

Akiongea na radio pinzani ya Power 105.1 katika kipindi cha "The Breakfast Club" Nicki amesema hakuwa amepanga kuperform single yake ya 'Starships' yenye mahadhi ya pop.


Baada ya sakata hilo, juzi kwenye kipindi chake Funk Master Flex alizungumza kwa simu na Nicki Minaj ili kuizungumzia issue hiyo na Nicki kuahidi kufanya show ya bure ili kuwalipa mashabiki waliochukia kutokana na kitendo chake cha kugoma kufanya show kwenye Summer Jam.

“Hakuna kitu kibaya kama kwenda nyumbani bila kufanya show. Nataka kuondoka kwa kusema: Nitawalipa mashabiki wangu. Na nataka mashabiki wangu wajue, hakuna, hakuna kituo cha radio, hakuna mtu atakayeubadilisha uhusiano wetu. Nina uhusiano wa karibu sana na mashabiki wangu, na ninaomba radhi sana kwakuwa niliuharibu usiku wa watu. Hamjui tu, nimepitia mengi sana. Mimi si mwachaji (quitter). Huwa naonekana na kuperform. Niliamua kufuata uamuzi wa timu yangu, na niliacha historia, na siku nyingine nikitoka, watu hawatanikosea heshima. Najisikia kama nimeuonesha ulimwengu, najipenda na kujiheshimu na watu hawatafikia huko tena. Na unajua nini, Flex? Tuwasiane kwa email, it's all good."

Katika hatua nyingine mpenzi wa Nicki Minaj, Safaree ametishia kumpa kichapo Peter Rosenburg watakapokuta uso kwa uso, " "YOOO PETER ROSENBURG WHEN I COME TO SUMMA JAM YOU GETTING PUNCHED IN YA F*CKING FACE U F*CKING P*SSY!!!!!!! I PROMISE U N*GGA!!!!!"

Rosenburg naye alizungumza na mtandao wa TMZ kuzungumza yake:

No comments:

Post a Comment