Monday, June 25, 2012

Wema Sepetu kumkutanisha Omotola Jalade na rais Kikwete





Muigizaji wa filamu nchini  Tanzania, Wema Sepetu amepanga kumkutanisha nyota wa filamu wa Nigeria Omotola Jalade na rais Jakaya Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam.

Omotola yupo nchini tangu wiki iliyopita alipokuja kwenye uzinduzi wa filamu ya Wema iitwayo Superstar.

Akiongea na XXL ya Clouds FM leo, meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda aka Survivor amesema lengo la wao kumkutanisha Omotola na rais Kikwete ni kufanya mazungumzo yatakayorahisisha biashara ya sanaa ya filamu kati ya Nigeria na Tanzania.

Amesema watamuomba rais Kikwete kupitia wizara inayohusika na masuala ya burudani kuweka utaratibu rahisi utakaosaidia wasanii wa Nigeria kuja nchini na wasanii wa hapa Tanzania kwenda Nigeria na lengo likiwa ni kukuza zaidi tasnia ya filamu nchini.
Wema,Omotola na Khadija Mwanamboka


Katika hatua nyingine Kadinda amesema filamu ya Superstaa inatarajiwa kuingia sokoni mwezi wa nane mwaka huu.

Ameongeza kuwa mpaka sasa wapo kwenye mazungumzo na wasambazaji watatu wakubwa nchini kuzungumza gharama za kuingia mkataba wa kuisambaza filamu hiyo.









Alipoulizwa kuhusu gharama waliyoiweka ili kuinunua filamu hiyo, Kadinda amesema ni kubwa kutokana na gharama nyingi za maandalizi na uzinduzi wake hasa kutokana na kumleta Omotola nchini.

Amesema watakapojumlisha gharama zote,watakuwa tayari kukitaja kiwango cha fedha wanachotaka ili kuiuza filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment