Friday, June 29, 2012

Chamber Squad wajipanga kupiga tour mwisho mwa mwaka



Ngwea, Dark Master, Noorah, Geez  Mabovu na Mez B wa kundi lililokaa kimya kwa muda mrefu la Chamber Squad, wanafikiria uwezekano wa kufanya tour ya pamoja mwishoni mwa mwaka huu.

Akiongea na East Africa Radio jana, Ngwea amesema pamoja na mipango ya kulikutanisha tena kundi hilo,yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Noorah aka Baba Stylez.

Ngoma hiyo iitwayo Chombeza Time imefanywa na mshindi wa tuzo za Kili mwaka jana kama producer bora Manecky wa AM Records.

Ngwea aka CowObama ambaye kwa sasa yupo jijini Mwanza, amesema kwenye ngoma hiyo ameamua kuimba huku Noorah akichana na amesema ni ngoma ambayo inaweza ikamrudisha poa yeye na Noorah.

Amesema hadi kufikia wiki ijayo ngoma hiyo ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua za mixing inaweza kuwa tayari kwenda hewani.

Kundi la Chamber Squad, ambalo zamani lilikuwa tishio limekuwa kimya, huku kila mmoja akifanya muziki kama solo artist.

Kwa muda mrefu Dark Master amekuwa akiishi jijini Mwanza ambako ameendelea kufanya muziki huko.

Noorah pamoja na kumaliza chuo na kupata kazi, mwaka jana aliachia ngoma iitwayo Lugha Gongana pamoja na video yake. Wimbo huo ulishirikishwa kwenye drama maarufu ya MTV Shuga ya nchini Kenya.

Kwa upande wa Mez B mwanzoni mwa mwaka huu aliachia ngoma iitwayo ‘Ring Tone’ iliyotengenezwa na Lamar wa Fishcrub lakini hata hivyo licha ya kuwa kali haikuhit sana.

No comments:

Post a Comment