Thursday, June 21, 2012

Exlusive with Audio: Shettah azungumzia familia, gharama ya video na collabo zijazo



Tumezungumza na Shettah mzee wa mdananda mambo kadhaa kuanzia maisha mapya kama mume wa mtu, gharama ya video ya wimbo wake mpya Nidanganye aliofanya na Diamond pamoja na collabo na ngoma mpya anazotarajia kufanya.

Kuhusu maisha mapya kama mume

Maisha ni mazuri na naenjoy kuwa mume. Mambo ya ujana yamepungua na vitu kama hivyo. Kutoka tena siwezi kutoka tena mara nyingi kihiyo. Nikitoka najua natoka naenda kufanya kazi. Zamani nilkuwa natoka sana, hakuna msanii nahisi aliyekuwa anatoka kama mimi.

Kuhusu gharama ya video ya nidanganye

Video kama video imenicost kama milioni tano ama milioni tano kasoro. Kitu chenye gharama zaidi ni mavazi sababu Adam mwenyewe bei zake zinajulikana ,ile nilimpa milioni mbili,  yeye hufanya video kwa milioni mbili milioni moja na nusu. Kwahiyo location, mavazi, usafiri safari cost za hapa na pale ndo zimefika kwenye tatu zingine, kwahiyo napigia kama tano hivi. Tulifanyia location pale Golden Tulip. Kila baada ya ,lisaa tulikuwa tunalipa laki moja na nusu na video yote imefanyika pale. Plus room, room ni dola 350 pale, kwahiyo tumepiga piga mahesabu ndo inakuja hiyo. Nakumbuka tulianza saa kumi jioni tulitoka pale saa tisa usiku ama saa kumi kasoro.

Kuhusu kama alimlipa Diamond kwa collabo hio

Diamond watu hawajui ni mtu wangu wa karibu nahisi kushinda wasanii wengine kwasababu wakili wale yeye ni wakili wangu mimi. Pia apart from that mimi na yeye tunaitana mapacha kwahiyo ni kama ndugu. Kuna vitu vingine tunafanyiana kama favour tu, so sikumlipa kitu chochote.

Kuhusu kama amerudisha gharama zake za video
Yeah ofcousre, sababu show moja milioni mbili, milioni mbili na nusu, hamna hamna moja nane kwahiyo isharudi.



Kuhusu collabo na nyimbo mpya

Nidanganye ni mpya sana bado kwasababu hata mwezi bado haijamaliza ama kumaliza ndo inaanza kumaliza sasa hivi. Kwahiyo this time tunajipanga tu na vitu vingine kwasababu msanii kama msanii lazima urekodi na vitu kama hivyo kwahiyo ninaplan kufanya wimbo na Wizzle na Radio wa Uganda. 

By the way nataka niende Kenya kufanya tu interviews za radio na TV na magazeti, kuna mtu anasimamia hiyo show kwasababu aliipenda hiyo nyimbo naye mwenyeji sana Kenya anaitwa Chief Kiumbe. Na kule ntakutana na wasanii wenzangu ambao wanafanya vizuri Kenya, kwahiyo nategema kufanya collabo na wasanii wa Kenya. Lakini kwa Tanzania pia kuna mtu anaitwa Ali Kiba, nshapatia beat kuna ngoma inabidi tufanye. Nimeongea na Gadner pia kuna wimbo inabidi nifanye na Lady Jaydee. Kwahiyo kuna project project sijajua kitu gani kanaweza kinaweza kikatokea katikati baada ya Nidanganye danganye!

Sikiliza interview yote chini.

No comments:

Post a Comment