Friday, June 22, 2012

Akon alipuuzia kumsainisha Drake kabla hajaenda YMCMB



Akon kwa hakika ana pua inayonusa vipaji, muulize tu T-Pain na Lady Gaga.

Lakini hata hivyo pamoja na kuwa hivyo kuna wakati huwa anashindwa pia kubaini madini na juzi kupitia kipindi "RapFix Live" rapper Kardinal Offishall aliweka wazi kosa alilolifanya.

"Nilimwambia kuhusu Drake mapema. Nilimwambia, Akon huyu dogo ni staa kwenye TV ni mkali balaa,” alisema Kardinall.


Kardinal Offishall alikiona kipaji na uwezo wa Drake kabla ya YMCMB.

Kardinal, kama Drizzy, Anatokea Toronto, lakini alifanikiwa kutoka kabla ya Drake hajafahamika mwaka 2009 na mixtape yake So Far Gone.

"Nilikutana naye kabla hajaanza kufanya mixtape yake ya kwanza,” alisema. Kitu ambacho nakumbuka kuhusu Drake ni kama alikuwa na njaa ya kutoka kwenye uigizaji kwenda kwenye kurap.”


"Baada ya kutoka nilienda na kumwambia Akon, “Nilikuambia”. Lakini hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yamefanya kazi kwa Drake na YMCMB. Ana kambi nzuri.”


Get More: Music News


Unahisi Drake angekuwa hapo alipo kama Akon angemchukua?

No comments:

Post a Comment