Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji Afrika Mashariki Tusker Project Fame msimu wa tano, limepata mchongo wa kuungana na miongoni mwa label kubwa kabisa duniani ya muziki Universal Music Group (UMG).
Hatua hiyo sasa itawaongezea nguvu zaidi washiriki wa mwaka huu katika safari ya kumsaka nyota mpya wa Afrika Mashariki.
Kutokana na ushirikiano huo, mshindi wa mwaka huu atakuwa na uhakika wa kufanikiwa zaidi kimataifa kwa kuwa chini ya usimamizi wa UMG.
Pia UMG itarekodi albam yenye nyimbo kumi ya washiriki kumi wa mwaka huu. “Wow...a whole 10 Track Album recorded by Universal Records for the Top 10 Contestants. So much at stake at #TPF5,” imesomeka tweet kwenye ukurasa rasmi wa Tusker Lager iliyoandikwa usiku wa saa 2 (June 23) wakati show ya live ikiendelea.
UMG, ambayo lengo lake ni kufanya kazi na wasanii wenye vipaji kutoka Afrika Mashariki na kuvikuza zaidi,imebaini kuwa Tusker Project Fame ni sehemu muafaka ya kuvipata vipaji hivyo.
Mshindi wa mwaka huu atapata bahati ya kufanya kazi na kampuni hiyo iliyofanikiwa duniani na ambayo inawasimamia pia wasanii wakubwa wakiwemo Rihanna, Lady Gaga, Justin Bieber, 50 Cent, U2, Youssou N'dour na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment