Tuesday, June 19, 2012

Interesting: Sasa unaweza kuoga bila maji na ukatakata!



Baada ya kubaini kuwa rafiki yake alikuwa mvivu wa kuoga na kutumia miezi michache kufanya utafiti kwenye internet, mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Afrika Kusini, Ludwick Marishane amekula shavu la ukweli baada ya dunia nzima kukubali ugunduzi wake ambao utafanya watu waoge bila maji!

Marishane, 22, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Cape Town amegundua bidhaa iitwayo DryBath, mafuta ya kupaka kwenye ngozi ambayo hufanya kazi ya sabuni na maji, watu wa Mbeya na Iringa mpoooo!

Ugunduzi huo uliomfanya Marishane ashinde tuzo ya Global Students Entrepreneur of the Year mwaka 2011, una faida kubwa barani Africa na maeneo mengine ya nchi zinazoendelea duniani ambako kuna uhaba wa maji unaowakabili mamilioni ya watu.


Marishane
Kijana huyo alikuja na wazo hilo alipokuwa kwao kijijini katika kipindi cha masika ambako rafiki yake alisema hawezi kuoga maji ya baridi kama hakutakuwepo maji ya moto kutokana na baridi kali nchini humo.


"Alikuwa mvivu na alikuwa anasema, kwanini mtu asivumbue kitu ambacho mtu utapaka tu mwilini bila kuoga,” alisema Marishane.

Marishane aliamua kutumia kimeo (simu) chake kilichokuwa na uwezo wa internet kusearch kupitia Google na Wikipedia katika kutafuta uchawi (formula).  Miezi sita baadaye alikuja na DryBath.


Mafuta hayo sasa yanatengenezwa kibiashara huku wateja wake wakiwa pamoja na mashirika makubwa ya ndege yanayoyatumia mafuta hayo kwaajili ya safari ndefu na pia serikali kwaajili ya kuwapa wanajeshi wawapo kazini.

DryBath moja inauzwa kwa dola 1.5 sawa na shilingi 2000 na kitu na mpaka sasa ameuza karibu mikebe 162,000.

Zawaidi aliyoipata kwa kupata tuzo ya Global Student Entrepreneur Awards ni dola 10,000 ambazo amesema atazitumia kwaajili kuitangaza zaidi bidhaa hiyo.

Marishane anasema bidhaa hiyo pia inasaidia kuhifadhi maji kwenye maeneo fukara duniani.

"DryBath will go a long way in helping communities".

No comments:

Post a Comment