Sunday, June 24, 2012

Grandmaster Records kumsaka mkali wa hip hop Arusha



Michano Entertainment(Grandmaster records) imeandaa mashindano ya rap mjini Arusha yatakayowashirikisha wasanii chipukizi.

Fainali za mashindano hayo zitafanyika siku ya Jumamosi ya June 30 mwaka huu.

Mshindi wa kwanza atakula shavu la kurekodiwa nyimbo mbili na video moja bure.

Usaili wa kuwatafuta wakali watakaochuana kwenye fainali ulifanyika June 16-17 mwaka huu ambapo masharti yalikuwa msanii awe na umri wa kuanzia miaka 18-25 na ambaye hajawahi kurekodi.

No comments:

Post a Comment