Tuesday, June 26, 2012

Wateja wa Vodacom kupata muda wa maongezi kwa kutumia M-PESA




Wateja kupokea muda wa maongezi wa shilingi 50 bure kila watumapo fedha kwa watumiaji wa M-Pesa waliojiandikisha.

Kampuni ya simu ya Vodacom leo (June 26) imezindua ofa ambayo itawafanya wateja wote wa M-pesa waliojiandikisha kupata muda wa maongezi kwa kila watumapo ama kupokea fedha.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Rene Meza ametangaza kutolewa kwa muda wa maongezi wa ziada wa shilingi 50 kwa wateja watakaotuma ama kupokea fedha kwa njia hiyo na kuongeza kuwa wateja wataweza kuutumia muda huo kupiga simu Vodacom kwenda Vodacom na kutuma ujumbe mfupi wa simu kwenda mtandao wowote nchini.

 “Jinsi mtu anavyotuma ama kupokea zaidi fedha kwa M-pesa, ndivyo atakavyopata zaidi muda wa maongezi wa ziada, alisema.

Meza amesema promotion hiyo ina lengo ka kuwatuza wateja wa Vodacom kwa kuendelea kuwa watumiaji wazuri wa mtandao huo.

“Promotion hii inaifurahisha Vodacom kwakuwa itawahimiza wateja wetu zaidi kutumia M-pesa na kuwaruhusu kuona jinsi M-pesa inavyoweza kubadilisha maisha yao wakati wakifurahia muda wa ziada wa maongezi na kutuma sms,” alieleza na kuongeza kuwa M-pesa inabakia kuwa miongoni mwa huduma muhimu zilizoanzishwa na Vodacom nchini Tanzania.

Karibu wateja milioni 3 waliojiunga na M-pesa nchini watanufaika na ofa hiyo.

No comments:

Post a Comment