Tuesday, June 26, 2012

Bodyguard wa Rihanna amtandika Paparazzi



Usiku wa jumapili  ya juzi mjini London, paparazzi mmoja aliambulia ‘jebu’ kutoka kwa baunsa aliyekuwa akimlinda Rihanna.

Ilitokea wakati Rihanna alipokuwa akitoka klabu ya usiku ya Whiskey Mist na kuzongwa na waandishi waliokuwa wakimmulika kwa flash za camera zao mithiri ya radi za usiku.

Hata hivyo bodyguard mmoja miongoni mwa mabodyguard lukuki waliokuwa wakimlinda Rihanna, alishindwa kuvumilia usumbufu huo na kumshushia ngumi paparazzi huyo iliyomfanya aunguke chini.

Hata hivyo wakati hilo linatokea Rihanna alikuwa ameshaingia ndani ya gari.

No comments:

Post a Comment