Friday, June 29, 2012

Jengo jipya la BBC- Broadcasting House, London ni nomaaaaaaaa!





“Siku ya mwisho kupiga kazi Bush House,” ni ujumbe kwenye mtandao wa Facebook ulioandikwa na mtangazaji mkongwe wa idhaa ya kiswahili ya BBC, Saleem Kikeke akiambatanisha na jengo la Bush house ambapo ndio makuu ya BBC London.

Muda mfupi tu baada ujumbe huo wa Kikeke maswali yakaanza kumiminika yakiuliza kama jamaa ndo anafungasha virago kurudi Bongo ama inakuaje! “Jaman ina maana ndo mwisho wa kisa na mkasa BBC?” ni miongoni mwa maswali mengi ya aina hiyo yaliyoelekezwa kwa Saleem Kikeke.


Jamaa alipiga kimya kwa muda pasipo kujibu lolote na kuwaacha mashabiki  wake na ‘mshawasha’ kuhusu hatma ya mzee wa kisa na mkasa.

Baada ya muda akaibuka na status nyingine kabisa. Awamu hii akaja na habari njema. “Tunahamia jengo jipya New Broadcasting House,” akiambatanisha na picha ya mjengo mmoja mpya na matata sana kwa mbali yakionekena maneno ‘BBC’!

Waliokuwa wamepanic kumkosa Saleem kwenye show yake maarufu ya kila jumamosi asubuhi kupitia BBC Swahili wakashusha pumzi na zikaanza kutolewa pongezi tu kwa maendeleo waliyoyafikia baada ya kuchoka kufanyia kazi ‘Bush House’.

Nasi tukapata hamu ya kulijua zaidi jengo hili. Ama kweli hili jengo ni maridadi. Sasa litajulikana kama ‘moyo wa London’.

Muda wa usiku taa zinapowashwa, unaweza ukadhani umetuwa kwenye casino maarufu za mjini Las Vegas, Mtoni.

Jengo linawaka haswaaaaa!

Jengo hili litakuwa na miongoni mwa nyumba vya habari (newsrooms) kubwa zaidi duniani.

Jionee mwenyewe!









“For the first time in our history we are bringing together the London headquarters of our News operations, our Radio operations and our Television operations in the most advanced digital broadcast and production centre in the world.”
Mark Thompson, BBC Director General

No comments:

Post a Comment