Wednesday, June 27, 2012

Happiness Magese: Matawi yake marefu sana siku hizi



Kwa muda mrefu Miss Tanzania mwaka 2001, Millen Happiness Magese amekuwa adimu kwenye midomo na vyombo vya habari vya Tanzania lakini yuko pazuri sana sasa hivi.

Akiwa kama model, Happiness kama ambavyo watanzania wengi wanamfahamu amesainishwa na kampuni za Ford Models in NY, NY na Ice Model Management mjini Johannesburg, South Africa.




Tangu awe mwanamitindo wa kimataifa ameshatokea kwenye cover za majarida mengi ya nguvu duniani kama Cosmopolitan, Ladybrielle, JCK (Ny), Uzuri, Bang, na Sawubona pia historia yake imeandikwa kwenye majarida kama Essence, True Love, Cosmopolitan, Elle, Opra, Marie Clare, Style, Glamour, na Wanted.





Pia amewahi kuonekana CNN na kufanya matangazo ya TV ya bidhaa kama Coke Light, JC Le Roux, Allan Grey, Guinness Milk Stout, Edgars, na Vodacom.





Kwa mafanikio aliyoyapata ameamua kujikita katika kusaidia watu wenye uhitaji hususan wanawake na watoto. Malengo yake makubwa ya baadaye ni kujenga shule ili watoto wa vijijini waweze kusoma kwakuwa anaamini kwamba elimu nzuri ni ufunguo wa maisha.



No comments:

Post a Comment