Mwanaume aliyeharibika vibaya mwili mzima kwa kutokwa 'madubashwa' ya ajabu na kupewa jina la "bubble man" ana matumaini kuwa huenda akapata tiba ya ugonjwa wake baada ya kukutana na daktari bingwa wa ngozi.
Chandra Wisnu anaumwa ugonjwa wa ngozi usiojulikana na kumtoa vipele vikubwa usoni na mwili mzima.
Baba huyo wa watoto wanne kutoka Indonesia,hutoka nyumbani mara chache sana na kama akitoka hulazimika kuficha uso wake kwa hofu ya kuogopesha watu ama kuzomewa na watu.
Chandra, 57, amesema madude hayo yalianza kutoka akiwa na miaka 19.
Akiwa na umri wa miaka 24 yalianza kusambaa mgongoni na alipofikisha miaka 32 yakaenea mwili mzima.
Baada ya kusikia story yake Dr Anthony Gapsari daktari bingwa wa ngozi kutoka Marekani aliamua kumsaidia Chandra.
Na sasa Chandra amepewa matumaini mapya kuwa ugonjwa wake unaweza ukapona.
No comments:
Post a Comment