Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba anatarajiwa kusaini mkataba na timu ya Shanghai Shenhua, na kuungana na Nicolas Anelka kwenye klabu hiyo.
Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast, 34, atatangaza uamuzi huo kwenye website yake binafsi.
Taarifa hizo zimetolewa na mwekezaji mkuu wa klabu hiyo Zhu Jun kwa shirika la habari la taifa la Xinhua.
Mkataba huo utamfanya Drogba alipwe paundi 200,000 ($314,000) kwa wiki.
Forward wa Ufaransa Anelka, aliyejiunga na Shenhua mwezi January naye akitokea Chelsea, aliwahi kuweka wazi kuwa angependa Drogba ajiunge na klabu hiyo ya kichina.
Hata hivyo Zhu amekanusha taarifa kuwa Drogba, aliyeondoka Chelsea baada ya kuisaidia klabu hiyo ya Ungereza kuchukua kombe la mabingwa wa ulaya mwezi uliopita kuwa atakuwa akilipwa, mshahara wa euro milioni 12 ($15.1 million).
Klabu hiyo tajiri ya Shenhua imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwachukua wachezaji wa ulaya na makocha pia. Katika msimu huu wamemfukuza kocha Jean Tigana na kumleta kocha wa zamani wa Argentina Sergio Batista mwezi uliopita.
Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya 12 kwenye ligi kuu ya China yenye timu 18.
No comments:
Post a Comment