Saturday, June 23, 2012

Exclusive: Joh Makini aongelea ‘Manuva’, Dunga, Weusi, shows na asichokipenda kwenye muziki



Joh Makini amerudi kwa kishindo na ngoma yake iitwayo Manuva na iliyotengenezwa na mtayarishaji mkongwe Ambrose aka Dunga.

Tumepiga story na Joh Makini aka Mwamba wa kaskazini kuhusu masuala mawili matatu kama ifuatavyo.

Kuhusu wapi aliporekodi Manuva, anapoishi na anachofanya producer Dunga

Manuva tumeifanyia pale kwa Dunga nyumbani  ana microphone yake, amegonga beat nyumbani ana monitors (speaker) kwahiyo tukafanya pale, halafu tukaenda kufanya final mixing na mastering kwenye studio za B’Hits kwa Hermy B. Dunga anaishi Mikocheni. Anafanya production na kazi zake binafsi.

Kuhusu wasanii wa Hip hop kutopiga show za hela kama wanazofanya wasanii wa kuimba kama Diamond

Mimi nafikiri hiyo ni kwa wadau tu ambao industry wanaiona hivyo lakini kwa upande mwingine nafikiri watu wa hip hop pia wengi wako smart sana kibiashara na watu wenye misimamo mara nyingi,  sasa hiyo kwenye industry inakuwa kama shida fulani hivi.

Kuhusu mipango ya Weusi

Weusi tuna hii albam yetu ya pamoja ya Weusi, baada ya hapo kila mtu anaenda solo sasa, lakini kampuni inabaki pale pale kufanya biashara za Weusi kama kuuza nguo za Weusi na cds.

Kuhusu kama biashara hizo zinawalipa

Yeah inatulipa, faida ipo kwasababu tunanunua bidhaa, tunaitengeneza,tunauza kwa kiasi fulani cha hela ambacho kina faida pale juu yake, na sio mbaya inatusaidia kidogo mafuta ya gari na vitu vidogo vidogo kuendesha maisha. Sisi t-shirt zetu tunaziuza kwenye maduka ya watu tu yaani kama Born 2 Shine, kwa CP jembe pale Mwenge kwahiyo tuna washkaji zetu wenye maduka, tukitoa mzigo tunawapelekea kwenye maduka yao kwasababu nao wanapenda kusupport hip hop, kwahiyo tunafanya nao biashara kwa style hiyo.


Kuhusu kitu asichokipenda kwenye muziki wa sasa

Upigwaji wa nyimbo kwenye radio stations, nyimbo zinakuwa hazidumu. Wimbo unatolewa, unapigwa wiki,unapigwa wiki inayofuata wiki nyingine zinakuwa hazipigwi tena. Yaani hakuna upigwaji ambao unaweza kuufanya wimbo uishi. Kuna ngoma kama za Hip hop usipozipiga mara nyingi watu hawawezi kuelewa sababu utakuta kuna metaphors,mle ndani kuna mashairi magumu, mtu anatakiwa ayasikike mara mbili, mara tatu ili aweze kuyatafakari na kuyaelewa. Nadhani tunahiji airtime nzuri kwaajili ya watu kuelewa hiki tunachokuwa tunakiongea kwenye mistari yetu tofauti na wasanii wengine wa kuimba sababu wao muziki wao unategemea tu melody sio katika uandishi. Kwahiyo watu wakishapenda melody basi wimbo unahit lakini wimbo wa hip hop kama watu hawajaelewa maishairi inakuwa kidogo kazi.

No comments:

Post a Comment