Thursday, June 28, 2012

Snoop Dogg akamatwa na bangi airport nchini Norway



Rapper mkongwe Snoop Dogg alikamatwa kwenye uwanja wa ndege nchini Norway leo baada ya maofisa wa uwanja wa ndege kugundua kuwa alikuwa akiweka bangi kwenye begi.

Polisi wameuambia mtandao wa TMZ kuwa Snoop alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Kjevic mjini Kristiansand ambapo maofisa waligundua kuwa alikuwa amebeba gramu 8 za ‘ganja’.

Kwa mujibu wa polisi, mtu akikamatwa na bangi iliyo chini ya gramu 15 huadhibiwa kwa faini peke yake na kwa kesi ya Snoop alitakiwa kulipa dola 1,980.13. sawa na zaidi ya shilingi milioni tatu.

Mtandao huo umeambiwa kuwa Snoop alionesha ushirikiano na kulipa faini haraka kwakuwa huenda alikuwa na pesa hizo mfukoni.

Snoop yupo nchini Norway kuperform kwenye tamasha la Hove.

No comments:

Post a Comment