Hatimaye msanii wa Bongo Flava Herry Sameer aka Mr Blue amepata mtoto wa kiume usiku wa kuamkia jana.
Akiongea leo kwa njia simu na Leotainment amesema ameamua kumpa jina lake mwenyewe la ‘Herry’ kwasababu ni mtoto wake wa kwanza.
Mr Blue amesema mchumba wake Wahda amejifungua kwa njia ya kawaida na wakati tunaongea naye kwa simu ndo alikuwa hospitali kukamilisha masuala kadhaa ili aruhusiwe (Wahda) kwenda nyumbani.
Akizungumzia mtoto wake anafanana na nani amesema, “ni mapema sana japokuwa naona sura imechanganyika huku na huku, sana naona kwenye macho amefanana na marehemu mother yangu, pia kwenye nywele naona kama mama yake, rangi naona yupo kwangu, kwahiyo nasikilizia akikua tuone itakuaje.”
Msanii huyo amesema mtoto wake akikua hapendi afanye muziki kama yeye kwakuwa hapendi awe maarufu.
“Mimi ningependa mwenyezi Mungu amjalie awe mtu fulani ambaye kidogo atakuwa hata kiongozi kusaidia watu,” alisema.
Sikiliza interview yote tuliyofanya naye hapo chini.
No comments:
Post a Comment