Sunday, June 24, 2012

Hatimaye: Beyonce & Kim Kardashian wakutanishwa hoteli kula dinner!



Kim na Bey wakishuhudia show ya Jay-Z na Kanye




Beyonce na Kim Kardashian wameweka pembeni tofauti zao na kujumuika pamoja kwenye chakula cha jioni mjini Birmingham, Uingereza wiki iliyopita.

Kim ana uhusiano na Kanye ambaye ni rafiki wa wote Beyonce na mume wake Jay-Z lakini kumekuwepo na taarifa kuwa Bey amekuwa akimkwepa Kim kwakuwa hafurahishwi na njia aliyoitumia Kim kuwa maarufu.

Inasemekana kuwa Kanye alipanga chakula cha jioni kwaajili ya warembo hao tu ili wafahamiane vizuri kwa kukaa pamoja kwa muda kwenye chumba cha hoteli.

"Wasichana hawa hawajahi kuonana macho kwa macho. Ni aibu kwakuwa Kanye na Jay-Z wako karibu mno. Beyonce siku zote amekuwa akimchukulia Kim kama nyota wa TV aliyejipatia umaarufu kwa kipaji mahsusi,” chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun.




"Kanye aliandaa dinner kwenye chumba cha hoteli kwaajili ya warembo hao kusawazisha mambo. Ana matumaini kuwa sasa wameshakuwa marafiki na hivyo kufanya wakutane tena sehemu zingine tofauti na ziarani. Beyonce amemkaribisha Kim kwenye ukoo.”

Na inaonekana mpango huo wa Kanye umefanikiwa tayari kwakuwa baadaye usiku huo Kim na Bey walionekana pamoja wakiwa na furaha huku wakiwaangalia ‘mashujaa’ wao (Kanye na Jay-Z) wakiendeleza makamuzi ya ziara ya 'Watch The Throne'.



No comments:

Post a Comment