Ukiwa waziri tena wa wizara nyeti kama wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na ukaamua kujiunga na Twitter, kuwa tayari kukoselewa, kupondwa na kupongezwa pia.
Mhe. Membe imemlazimu kwenda na wakati na sasa ameshakuwa mwenyeji wa Twitter. Akiwa kama waziri wa masuala ya nje ni halali awepo huko ili aendane na ulimwengu wa mitandao ya kijamii.
Kujiunga kwake kumewapa mwanya wale waliokuwa wakitamani kumuuliza maswali yao ama kusema yaliyomo moyoni kuhusiana naye,wanaitumia vema fursa hiyo.
Haya ni miongoni mwa masuala aliyoulizwa leo baada ya kuongea kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM.
Fred Kavishe: Wanaonichafua wanajifahamu"si uwataje??kuwa muwazi na uraisi vipi?
Membe: Nchi kwanza urais baadae. Tunalo jukumu la kujenga nchi kwa sasa na si kujadili urais wa 2015
Fred Kavishe: Okay, nimekuelewa Mr. tujenge nchi yetu sana na mpunguze safari za nje zisizo na tija kwa taifa.
Membe: Hatufanyi safari zisizo na tija, isipokuwa zipo zile ambazo manufaa yake yanaonekana ktk muda mfupi na yale ya muda mrefu.
Salim saitoti: nakusikiliza unavyojigamba kama pesa ya rada imerudi, HATUITAKI, tunamtaka aliyeipeleka
Membe: Jukumu la Wizara yangu ilikuwa ni kuhakikisha fedha inarudi nchini na nimefanya hivyo kwa kushirikisha Bunge na zimerudi zote.
Allen Mushi: Kwahiyo dhana ya kusema Kaskazini wanapendelewa au wana maendeleo na wengine hawana ife koz kama huchapi kazi utakua masikini!
Membe: hayo ndio mawazo ya kuigawa nchi ambao tunapaswa kuyapiga vita.Hakuna kati yetu aliye bora kuliko Tanzania.
Gerald Nyerere: Tumekusikia Mheshimiwa, Ila sie Chadema, tutawapiga bao, si kwenye bajeti tu, hata kwa maendeleo ya nchi (committed responsibilities)
Membe: Siasa ya ushindani ndiyo nayoiamini.
No comments:
Post a Comment