Saturday, June 23, 2012

Albam ya Usher kuuzwa Nigeria kwa mara ya kwanza katika historia





Sony Music Entertainment Africa imeingia mkataba na kampuni ya MComm ( kampuni kubwa ya burudani inayoongoza nchini Nigeria) kuipeleka ‘rasmi’ albam ya Usher “Looking 4 Myself kwenye maduka ya muziki ya Nigeria.

Huo ni ushirikiano wa pekee, Nigeria ikiwa nchi ya kwanza ya Afrika Magharibi kuwa na uzinduzi rasmi wa albam kutoka kwa msanii huyo mshindi wa tuzo za Grammy, na utaunda msingi wa ushirikiano mwingine na kampuni ya Sony Music.

Albam hiyo itapatikana nchi nzima kama sehemu ya uzinduzi rasmi ikiwa kwenye mfumo wa Compact Disc (CD) na itauzwa kulingana na soko la Nigeria.

Looking 4 Myself itapatikana kwenye majiji makubwa ya Lagos, Abuja, Port- Harcourt, Enugu na itapatikana mitaani, kwenye maduka ya nyimbo na mawakala.

Albam hiyo itazinduliwa rasmi jumatatu ya kesho kutwa nchini humo na tayari nyimbo tatu zimeshaachiwa ambazo Climax, Lemme See na “Scream”

No comments:

Post a Comment