Wednesday, June 20, 2012

Beyonce amwandikia barua shabiki wake kipofu




Beyonce amemwandikia barua ya wazi shabiki wake Timmy Kelly, aliyezaliwa na upofu wa macho.

Mwanamuziki huyo alikutana na Timmy kwa mara ya kwanza wakati kijana huyo akiwa na miaka 13, backstage kwenye tuzo za Grammy.

Timmy kidogo amlize Beyonce baadaya kumwimbia wimbo wake Irreplacable, na hamjamsahau hadi leo.


Baada ya kubaini kuwa Timmy ambaye kwa sasa ana miaka 18 amehitimu high school na amechaguliwa kujiunga na chuo, Bey ameandika barua ya kumpongeza kwa hatua hiyo.

“Mara ya kwanza nimekutana na Timmy ilikuwa mwaka 2007, backstage kwenye Grammys. Alikuwa na miaka 13 na aliugusa moyo wangu kwa sauti yake na mapenzi yake kwa muziki na maisha,” ameandika Beyonce.

“Sasa hivi ana miaka 18 na amehitimu high school – Najinua sasa kwake!”
"Timmy alizaliwa kipofu. Lakini hili halikumtatiza. Amethibitisha kwa kila mmoja kuwa kila kitu kinawezekana kama ukijiamini na kujituma.” 

"Mjini Philadelphia anajulikana sana kama bahati kwa Eagles na kila anapoimba wimbo wa taifa kwenye mchezo timu hiyo hushinda.”

"Uwezo wake na kujituma kwake unavutia. Timmy alikubaliwa kujiunga na chuo kikuu cha Boyer kusoma muziki na dance.”

“Hongera Timmy, Love, B."

No comments:

Post a Comment