Wednesday, June 27, 2012

Download: Belle 9 na Ben Pol – Anayeishi Naye



Hatimaye ngoma ya wakali wawili wa chorus Tanzania 2010 -2012 kwa mujibu wa leotainment umetoka rasmi leo. Belle 9 na Ben Pol wamekutana pamoja na kufanya ngoma hii iitwayo ‘Anayeishi Naye’ ambayo imetengenezwa na Mona Gangster.

Kisa kwenye wimbo huu ni kuwa wote walikuwa wakitoka na dem mmoja ambaye aliwakuwa akiwachanganya bila wao kujijua. Lakini baadaye wakaja kugundua kuwa kumbe kila mmoja alikuwa akiambiwa na demu huyo anampenda kwa dhati, wakati sio.

Wanasikika wakiambiana kuwa ‘siku zote hizo ulizokuwa naye kumbe amekudanganya! Wote wamekuja kugundua kuwa pamoja na demu huyo kuwachanganya na kuwaahidi ‘vinono’ amempata mwanaume mwingine anayeishi naye na wao wakipigwa chini.

Story inataka kunafafa na ‘Same Girl’ wa Usher na R.Kelly japo Belle na Ben wamekuja kuachwa wote na kubaki losers!

Ni wimbo mkali nasi tunaupa mic 4 za kuanzia!


No comments:

Post a Comment