Baada ya kukaa kimya kwa muda tangu atoe wimbo wake uitwao ‘Hata Kwetu Wapo’, Tumeongea kwa simu na Sam wa Ukweli kutaka kujua nini kinaendelea.
Kuhusu kwanini amekaa kimya
Ule wimbo wa ‘Sina raha’ na ‘Hata kwetu wapo’ ulikuwepo kwenye ile project ya kwanza, albam ya mwanzo kabisa. Sasa nikapata tena mchongo wa kufanya albam nyingine, kwahiyo nikawa busy kidogo na studio na majukumu ya kifamilia, nikawa najaribu kuweka mazingira sawa. Halafu vile vile menejimenti niliyokuwa nayo mkataba wake ulipoisha nikawa nafuata process za menejimenti nyingine kwakuwa kuna wasanii wengine niliwakuta, nikawa navuta subira angalau nafasi yangu ifike, ndo hii imefika sasa hivi.
Kuhusu tofauti kati ya nyimbo za mapenzi na nyimbo za mambo ya jamii
Kikubwa unajua mapenzi yapo siku zote. Na ndo maana hata nyimbo nazotaka kuwaimbia jamii, nataka niimbe kitu ambacho kwenye miaka na miaka watu wanaweza wakakizungumza kama navyozungumza kwamba hata kwetu wapo, kitu kidogo kinaweza kikatokea mtu mwingine anaweza akasema “sio kwenu tu juzi sisi kwetu kilitokea.” Kwahiyo najaribu kidogo kutofautisha sababu mapenzi yamechukua jamii nzima. Lakini unaweza kukuta umeimba wimbo wa jamii ukakuta kuna watu umewagusa wengine hawana hizo habari kwasababu kuna watu wanaishi maisha mazuri tangu wazaliwe hawajui kama kuna shida ama dhiki. Lakini mapenzi ukiwa tajiri ukiwa masikini yatakukuta na utakuwa nayo sababu hakuna mtu anayekosa mahusiano.
Kuhusu tofauti kati ya menejimenti ya mwanzo na ya sasa
Utafauti upo kwasababu ukizungumzia Aljazeera ni menejimenti ambayo imewatoa wasanii wengi kama Sameer. Kwahiyo kwenye industry ya music ina mizizi mingi tofauti na awali ambapo nilikuwa na kaka yangu Kisaka kwasababu tulikuwa tunajiendesha sisi kama sisi, hatukuwa na capital hiyo kusema kuweza kuwekeza saNa kwenye music, lakini ni mwenyezi Mungu tu ametusaidia mpaka tumefika pale. kwahiyo kuna utofauti, kisaka ni producer atadeal sana kwenye uprodusa na mimi kama mwanamuziki ntadeal kwenye mashairi. Aljazeera kila mtu ana section yake kuna mhasibu, kuna mwingine anafanya promotion ,kuna mwingine kama Mkurugenzi, kuna mwingine kama designer kwahiyo ni menejimenti ambayo ina matawi mengi.
\
Kuhusu gharama ya show zake
Show zangu mimi nafanya kwa milioni 3.5 baada ya video hii mpya ntapandisha mpaka milioni tano sababu nategemea kupata promotion ya maana. Unajua muziki kwakweli namshukuru Mungu umebadilika tofauti na awali. Kwa sababu kaka zetu akina Sugu akina Nature walikuwa wanafanya show kwa laki tano, laki sita. Lakini sasa hivi muziki umebadilika kwasabbu hata mimi mwenyewe nakumbuka show yangu ya kwanza kufanya nililipwa laki nane.”
Kuhusu alichokipata tangu aanze muziki
“Sasa hivi mimi nina mji wangu namshukuru Mungu. Ninafamilia yangu, nina sehemu ya kujificha, nina kabanda ambapo leo kesho hata kama muziki hautakuwepo, kuna kitu ambacho ninacho na kinafanya mpaka kesho na kesho kutwa nitaendelea kukaa. Namshukuru Mungu mambo yanaenda mjini, kwamba zile habari ambazo zamani nilikuwa nasema ntakodi taxi, ntakodi bajaj, lakini sasa hivi nashukuru Mungu, ninacho kidogo kidogo nina drive.
Ili kusikiliza mengine aliyoyazungumza kwenye interview hii bonyeza hapo chini.
No comments:
Post a Comment