Wednesday, June 27, 2012

Capital Fm Kenya: Wasikilizaji wachache, hela nyingi! Siri yake itaziamsha radio za Bongo



Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa na mtandao wa Ghafla wa Kenya kuhusiana na survey iliyofanywa na KARF ya robo ya mwaka 2012, Capital FM haina wasikilizaji wengi kihivyo.

Mtandao huo umesema linapokuja la kugawana soko la usikilizwaji wa radio, survey hiyo imeonesha kuwa Capital inamiliki asilimia 0.3% tu. Licha ya hilo Capital FM bado imeendelea kuwa na gharama kubwa za matangazo. Kwa kawaida wengi watakuwa na imani kuwa radio yenye wasikilizaji wengine ndio itakuwa na gharama kubwa!

Habari ni kwamba dunia ya matangazo imebadilika sana siku hizi na kutumia zaidi formula iitwayo Living Standard Measure(LSM). LSM inahusiana na kiwango cha utajiri, furaha, kuridhika, umiliki wa vitu na vitu muhimu vilivyopo kwenye class fulani ya kiuchumi katika jamii.

LSM inapimwa katika level zifuatazo.

LSM 1-3 = Maskini
LSM 4-6 = Wenye uwezo wa kati
LSM 7 and 8 = Wenye uwezo wa juu kidogo
LSM 9 and 10 = Matajiri

Capital wamejiweka kwa makusudi kuchukua soko la level ya LSM 9-10 ambalo lina wananchi wakenya waishio kwenye maeneo ya watu wazito kama Karen na Muthaiga, ambako pamepewa jina la “barbies.”

Ukweli unaochukiza ni kuwa kwenye ulimwengu wa matangazo, makampuni yanayotangaza huwathamini matajiri kuliko wenzetu na sisi maskini. 

Huzingatia uwezo na utayari wa kununua zaidi. Fikira za wenye matangazo ni kuwa wanataka kuuweka ujumbe wao mbele ya watu ambao wanaweza kununua bidhaa zao na hivyo huona ni bora kutumia fedha nyingi kutangaza kwa watu wazito wanaosikiliza radio hiyo.

Hivyo linapokuja suala la watu maskini wanaosikiliza radio zingine, makampuni huwa hayaamini kama wanaweza kununua bidhaa zao kwa wingi, kwahiyo hulipa pesa kidogo kupeleka ujumbe kwa ‘makapuku’

Ndo maana hata hapa Tanzania, Choice Fm ambayo ina wasikilizaji wachache, bado ina matangazo lukikU kwakuwa inasikilizwa na watu ‘mambo safi’!

No comments:

Post a Comment