Saturday, June 30, 2012

Exclusive: Sikiliza igizo la MTV Shuga Radio EP.1 Kiswahili hapa



Ile Drama ya MTV Shuga: Love, Sex, Money inatarajia kuanza kusikika kwenye vituo vya radio jumatano ijayo katika nchi sita.

Show hiyo ya runinga iliyojishindia tuzo, imewekwa kwenye mfumo wa radio ili kuwafikia wasikilizaji wa radio zaidi ya milioni 45 katika nchi za Cameron, DRC, Kenya, Lesotho, Afrika Kusini na Tanzania.

Show hiyo ya radio imetengenezwa kwa lugha mbalimbali ambapo wasikilizaji wa Tanzania na Kenya watakuwa wakisikiliza version ya Kiswahili.

Mradi huo unaungwa mkono na Unicef, MTV Staying Alive Foundation, US President's Emergency Plan for AIDS Relief na the Partnership for an HIV Free Generation kwa ushirikiano na vijana, wawakilishi wa serikali na wadau kutoka kwenye nchi zinazoshiriki.

Shuga Radio inahusisha story za vijana wenye umri kuanzia miaka 15-24.
Mfululizo wa show hiyo unasimulia machaguo ya vijana hao, ndoto zao, urafiki, changamoto na ushindi katika dunia ambayo virusi vya HIV na Ukimwi ni tishio kubwa.

Shuga Radio itaangalia masuala yale yale yanayotazamwa kwenye show ya TV yakiwemo ushauri nasaha na kupima, matumizi ya condom kwenye mahusiano imara, kujikinga, utofauti wa kijinsia na ukatili wa kimapenzi, ulevi na mambo mengine.

Washiriki utakaowasikia humu ni Amina,Fally,Sharon,Feruz, Karis na Riziki.

Isikilize kwa mara ya kwanza hapa:

No comments:

Post a Comment