Thursday, June 28, 2012

Camp Mulla washindwa kupata visa mapema, wanaweza kuzikosa tuzo za BET



Kundi la Camp Mulla linaweza kujikuta likisubiria nyumbani habari za kama limeshinda tuzo kwenye kipengele cha Best International  Act Africa ya BET baada ya kuchelewa kushughulikia visa kwaajili ya kusafiri kwenda nchini Marekani kuhudhuria.

Kwa  mujibu wa ripoti ambazo hazijathibitishwa,vyanzo vya nchini Kenya vimedai kuwa kundi hilo limeshindwa kushughulikia visa mapema kwa ajili ya kusafiri kwenda kuhudhuria  tuzo hizo. 

Inasemekana baada ya kuchelewa, waliamua kuomba visa maalum kwa kuweka sababu ya kuwa wametajwa kwenye tuzo kubwa duniani. Visa maalum hutolewa kwa wale wanaosafiri kwasababu za ugonjwa, kutafuta hifadhi za kisiasa ama safari za kiserikali.

Waliamua kwenda kwenye interview mapema kabla ya tarehe waliyokuwa wamepangiwa lakini waliambiwa kuwa haiwezekani kufanya kabla ya tarehe husika.

Hivyo kundi hilo linaweza kupata visa lakini baadaye sana ambapo tuzo hizo zitakuwa zimeshatolewa.

Tuzo za BET mwaka huu zitafanyika jumapili hii, July 1 huku MC akiwa muigizaji wa filamu, Samuel  L Jackson.

No comments:

Post a Comment