Monday, June 18, 2012

Issue ya Kitaifa: Waziri Membe atweet ujumbe kwa CHADEMA


   
Leo katika mtandao wa Twitter tumekutana na tweets nyingi za waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe zenye ufafanuzi juu ya suala muhimu kuhusu upinzani na CHADEMA.

Kwakuwa yeye mwenyewe pia amejiunga hivi karibuni tu katika mtandao wa Twitter tumeona si mbaya watu wakafamu nini alichokiandika kwakuwa ni suala linalohusu mshikamano na umoja wa watanzania.

“Nimefafanua kuhusu uvumi uliotolewa na vyombo vya habari kuhusu kukutana kwangu na vijana wa CHADEMA waliofika nyumbani kwangu jimboni. Nimewaeleza kuwa upinzani si uadui na wapinzani si maadui zetu.

Sijawahi kuitabiria CHADEMA ushindi kwa kuwa sina kipaji hicho ambacho kinapatikana kwa Synovate, Mtoto wa Sheikh Yahya na TD Joshua

Nina imani uvumi huu haujaenezwa na CHADEMA bali watu nje ya CHADEMA wenye malengo ya kisiasa haswa kunifitinisha na wana CCM na CHADEMA

Upinzani upo kwa mujibu wa kanuni, sheria na Katiba hivyo hauwezi kuwa uadui. Wapinzani wako ndani ya vyama vyetu wenyewe

Kamwe watanzania tusikubali kulishwa kasumba ya kuwa Upinzani wa kisiasa ni uadui. Tusigawanywe kwa itikadi wala dini.

Nawapenda watanzania wote bila kujali itikadi zao, dini zao, makabila yao na marika yao. Umoja wetu ndio nguvu yetu.

Mimi ni mwana CCM kwa mawazo, kw maneno na kwa vitendo. Na nitaendelea kuwa hivyo hadi Mungu atakaponichukua.”

Uamuzi wa Mheshimiwa Membe kutoa ujumbe huo mzito kupitia Twitter unaonesha jinsi mitandao ya kijamii inavyozidi kutumiwa na wanasiasa kuzungumza masuala ambayo ingekuwa ngumu kufanya hivyo kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment