Tuesday, June 26, 2012

Mpaka leo wapo wanaodhani Mt.Kilimanjaro upo Kenya?




Hivi karibuni mcheza filamu na mrembo wa Marekani Deirdre Lorenz alitua mjini Moshi kwaajili ya mapumziko na pia kuushuhudia mlima Kilimanjaro.


Muigizaji huyo anayejulikana kwa filamu kama 'Perfect Strangers, Santorini Blue na Big Fight alitua Tanzania kwa Ethiopian Airline kushiriki mbio za marathon zilizofanyika June 24.

Jambo la kushangaza mpaka leo hii ni kuwa mwanadada huyo alikuwa anajua kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya. Alisema alishangaa kuja kuukuta upo Tanzania.

Lawama hii moja kwa moja inaenda kwa wizara ya maliasili na utalii kupitia idara ya utalii Tanzania ambayo imeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo katika kuutangaza mlima huu.



Lakini katika dunia ya leo ni jambo la kushangaza sana kwamba bado kuna watu wameendelea kufahamu mlima huu upo Tanzania.

Japo si rahisi kwa mtu kuamua tu kugoogle ili kujihakikishia mahali mlima huo ulipo, ni ujinga kwa raia wa nje kuendelea kufikiria hivyo wakati mtandaoni kuna kila taarifa muhimu kuhusu mlima huo.

Hata hivyo mrembo huyo amesema akirudi Marekani atakuwa balozi mzuri wa kutangaza mahali halisi mlima Kilimanjaro ulipo yaani Tanzania.


No comments:

Post a Comment