Thursday, June 28, 2012

Ay asema hatochukua nyimbo zilizosalia B’Hits, ataandika upya





Msanii wa hip hop na mwimbaji nchini Tanzania Ambwene Yesaya aka Ay amesema hana mpango wa kuzichukua nyimbo zilizosalia B’Hits.


Ay amesema hayo wakati akihojiwa leo kwenye kipindi  cha Power Jams cha East Africa Radio japo amesisitiza kuwa atatoa taarifa rasmi ya kujibu barua za Hermy B ambazo zote ziliandikwa hapa exclusively.

Katika barua ya kwanza ya Hermy B alidai kuwa baada ya Ay kutokubaliana na gharama mpya ya kurekodia ya shilingi milioni 2 kwa wimbo, Ay alikaa kimya kiasi kilichomfanya (Hermy) amwambie azifuate nyimbo zake ambazo angempa bure. Hermy alisema kwa zile nyimbo ambazo hazijafanyiwa mixing itabidi Ay akazifanyie kwenye studio nyingine.

Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo mafupi ya Ay aliyoyatoa leo kwenye Power Jams ni kwamba hana shida tena na nyimbo hizo na ameanza kurekodi upya.

Ametolea mfano wimbo wake mpya unaohit sasa hivi wa ‘Party Zone’ ambao video yake ina gharama kubwa kuliko zote zilizowahi kufanywa na msanii wa Tanzania, pamoja na wimbo walioperform na MwanaFA walipoalikwa kwenye Big Brother Afrika mwezi huu uitwao ‘money’.

Amesema pamoja na kwamba nyimbo hizo hatazichukua, bado ataendelea kuwa na haki ya mashairi yake ambayo akipenda anaweza kuyabadilisha zaidi na kurekodi studio anayoitaka, huku Hermy B akisalia na haki ya umiliki wa beat peke yake.

Mzee huyo wa commercial ameongeza kuwa hakuna mtu yeyote anayemsimamia na ana uhuru wa kufanya kazi na studio yoyote ndani na  nje ya nchi.

Hata hivyo amesema hawezi kubeza mchango wa B’Hits katika career yake lakini akaongeza kuwa wao pia (yeye na MwanaFa) wameiweka kwenye ramani studio hiyo, kitu ambacho Hermy B alikikubali kwenye barua aliyotuandikia.

Ambwene amesema tangu kuacha kurekodi B’Hits hajaona madhara yoyote kimuziki ama kibiashara na kazi zinaendelea vizuri kama kawaida.

Amesema kwa sasa yeye na MwanaFa wako busy kidogo na pindi wakitulia watakaa chini wote kwa pamoja kutoa maelezo yao rasmi na kujibu barua ya Hermy B.

No comments:

Post a Comment