Tuesday, June 26, 2012

Billionare atoa ofa ya $mil.3 Drake na Chris Brown waingine ulingoni



Promoter wa ndondi nchini Marekani Damon Feldman ameliambia gazeti la NY Daily News kuwa billionare Alki David yuko tayari kuweka mezani dola milioni 3 ili Drake na Chris Brown waingine ulingoni kuzichapa kweli kweli.

Kila mmoja atachukua dola milioni moja na inayosalia itaenda kusaidia vituo vya misaada.

Feldman amesema kama likiwepo, pambano hilo la kulipa ili uangalie ‘ pay-per-view’ litafanyika Las Vegas ama Los Angeles, August 25.

“Ni wazi kuwa wanachukiana. Litakuwa pambano la round 3 tu na kila moja ikiwa na dakika moja. Hakuna atakayeumia sana,” Feldman aliliambia gazeti la Daily News.

Mwakilishi wa Breezy anadai kuwa bado hajapokea ofa rasmi.

Feldman alisema angependa Rihanna awe sehemu ya pambano hilo pia.

“I would love to have Rihanna as the ring girl.'


Kama kweli likifanyika hili litakuwa pambano la mwaka, nani unahisi atanyukwa?

No comments:

Post a Comment