Saturday, June 23, 2012

Soggy, Misosi na D-Knob kupiga tour ya hip hop


Soggy


Wasanii wakongwe wa hip hop nchini Soggy Doggy,Bwana Misosi na D.Knob wanarajia kufanya ziara ya pamoja katika mikoa ya kanda ya ziwa, Ruvuma na Arusha mwezi ujao.


Kwa mujibu wa Soggy ambaye pia ni mtangazaji wa Uhuru Fm, ziara hiyo iliyodhaminiwa na PRO-24 imeandaliwa kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wao ambao huwa wanawaona mara chache kutokana na kubanwa na majukumu mengine.


Katika ziara hiyo wasanii hao waliotamba na vibao kama Kibanda cha simu, Nitoke vipi na Sauti ya Gharama wataambana na madansa wao kunogesha show yao.

Misosi

No comments:

Post a Comment