Tuesday, June 26, 2012

Iryn Namubiru wa Uganda alipwa zaidi ya mil 4.7 (tshs) kwa show ya wimbo mmoja




Mwanamuziki wa kike wa nchini Uganda Iryn Namubiru wiki iliyopita alikamata mkwanja mrefu alioupata kiulini kabisa.

Kwa malipo ya dola 3,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 4.7 za Tanzania aliperform wimbo mmoja tu uitwao ‘Happy kwenye cocktail ya watu wazito pale Sheraton Rwenzori Ball Room, Kampala Uganda.

Alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Happy Science, dini ambayo ilianzia nchini Japan na kuwaalika waumini wake kwenye hoteli hiyo.

Dini hiyo yenye waumini milioni 12 katika nchi 90 duniani, itamleta muanzilishi wake Ryuho Okawa barani Africa kwa mara ya kwanza ambaye atahutubia kwenye uwanja wa Namboole.

Ryuho Okawa
Jose Chameleone, aliyeutunga wimbo huo Happy People na producer wa studio ya Swangz Avenue, Benon Mugumbya nao pia walikamata mkwanja mrefu ambao hata hivyo haukujulikana mara moja.

No comments:

Post a Comment