Saturday, June 23, 2012

Hakuna mtanzania tena kwenye Tusker Project Fame 5


Damian


Let’s face it! Pamoja na kuwa mashindano ya mwaka huu ya Tusker Project Fame yameongoza kwa kuwa na washiriki wabovu, wasiojua kuimba na wenye vipaji vya mashaka,Tanzania imeongoza.


Kama umepata bahati ya kuwaona watanzania walivyokuwa wanahangaika kuimba jukwaani utakuwa umejiuliza waliwezaje kupita kwenye auditions?

Wasanii wabovu kabisa! Ndo maana wametoka mapema,hakuna uonevu.

Leo mshiriki wa mwisho kutoka Tanzania, Damiani Innocent Mihayo amefungasha virago na hivyo Tanzania kutokuwa na mshiriki tena. Hiyo ina maana kuwa mashindano ya mwaka huu tutabakia kuwashuhudia tu  washiriki kutoka Uganda, Kenya, S. Sudan, Rwanda na Burundi.

Pamoja na mwaka huu shindano hili kuwa na vinono vingi kuliko mashindano yote yaliyopita kama vile kuingia kwa Samsung kusaidia masuala kadhaa ya kiteknolojia husasan simu za Samsung Galaxy, Universal Music Group nao wameingia kuweka nguvu.

Watanzania wameichezea fursa hii ya kipekee ambayo kama tungepeleka washiriki wazuri tungepata nyota mwingine mkubwa wa kimataifa.

Inauma sana!


No comments:

Post a Comment