Wednesday, June 27, 2012

Baada ya Rick Ross, P-Square kupiga ngoma na Drizzy Drake



Peter na Paul Okoye, P-Square,  hawataki mchezo kabisa sasa hivi. Baada ya kumweka Rick Ross kwenye remix ya Beautiful Onyinye na akatambaa nayo fresh, sasa wanajaribu kuona kama wanaweza kupiga ngoma na mwana YMCMB, Drake.

Haijathibitishwa rasmi lakini picha hii iliyowekwa kwenye page yao ya Twitter inaashiria kuwa very soon watapiga ngoma na mkali huyo.

Kama wameweza kupiga ngoma na boss wa Maybach Music, si kazi ngumu kumpa shavu Drizzy kwenye ngoma yao mpya.

Yetu macho na masikio.

No comments:

Post a Comment