Thursday, June 28, 2012

Mfahamu Octopizzo rapper aliyezindua condom zake





Kuna wale ambao sasa hivi nchini Kenya wanamuona kama rapper bora kabisa kuliko wote. Kila ngoma anayotoa inamsogeza zaidi kwenye kulimiliki taji la king wa rap wa Kenya. Kijana huyu anatishia nafasi za wakali kama Collo na Abbas kwenye hip hop ya nchini humo.

Kwa sasa amekuwa gumzo nchini Kenya kwa kuzindua condom zake ziitwazo ‘let’s do it.



Kwa wale ambao wameshazitumia wanasema zimewapa mizuka ya ajabu. Kinachofurahisha ni kuwa condom hizi zinatoa mwanga ama zinawaka gizani.


Leo kupitia Twitter amesema condom hizo zitaingia sokoni hivi karibuni, "the first stock should be here in a months time what will take time is formalitiz and ish."

Anaamini kuwa katika dunia yale leo si rahisi kumwambia kijana aachane kabisa na ngono ili kuepuka virusi vya HIV hivyo ni afadhali kama wakitumia condom. Leo (June 28) ametweet, “in the 21st century telling a teenager or a 21yr old to abstsin ni ka kudial 555 and telling zack "we not brunging yu home"

OCTOPIZZO NI NANI?

Ni msanii wa hip hop kutoka Kibera, eneo maarufu sana jijini Nairobi wanapoishi watu wa hali ya chini kabisa, akina kajamba nani (the largest slum in Africa).

Ni mhasisi wa kundi la vijana liitwalo Y.G.B. (Young, Gifted, and Black), likiwa na rapper wenye vipaji, watunzi wa mashairi, wachoraji, wasanii wa graphics na dancers.

Alizaliwa mwaka 1987, kwa jina la HENRY OCHIENG. Amesoma shule ya msingi na sekondari hapo hapo Kibera pamoja na St. Mary's Changamwe College mjini Mombasa,kabla ya kurejea Nairobi kujaribu bahati yake ya muziki.

Akiwa na Prezzo

Ni mtoto wa kwanza kwenye familia yao ya watoto wanne na pia ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy.

Akiwa na umri mdogo kabisa Octopizzo alifunzwa na maisha magumu ya Kibera lakini kuvutiwa kimuziki na wasanii kama Chino XL, Big L, KRS, Diabolic, EPMD, Copyright, CL Smooth, Immortal Technik, na Supernatural.
Ameshinda mashindano kibao ya freestyle nchini Kenya, kama G Pange Hip Hop Challenge, Hip Hop Halisi Freestyle Challenge, na Usanii Kona Hip Hop Challenge.



Octopizzo ameshapanda kwenye stage moja na wasanii wa kimataifa kama Dead Prezz (U.S.A.), Black Twang (U.K.), DJ Trouble Maker (U.S.A.), Bunt Face (U.S.A./Ethiopia), Malikah (Lebanon), Le Melanina (Colombia), Mad Maxamon (Germany), Restley Perez (Philippines), na Anne Khan (Germany). Na pia ameshaperform na wasanii wa Kenya wakiwemo Jua Cali, Nonini, P Unit, Wahu, Wyre, Jaguar, Jimmy Gait, Ukoo Flani, Point Blank, Mwafrika na Ness.
Mpaka sasa amesharekodu mixtape tatu, S.O.N. (Stragglers of Nairobi), Y.G.B. (Young Gifted and Black), na The White Shadow. Mwkaa 2008 S.O.N. ilikuwa mixtape iliyouza zaidi katika historia ya hip hop ya Kenya.



Pamoja na muziki, Octopizzo ni mwenyekiti mtendaji wa Chocolate City (Kibera) Tours na mwenyekiti na mwanzilishi wa Y.G.B. (Young, Gifted, and Black)

Pia ni muigizaji na ameshaonekana kwenye show ya MTV SHUGA msimu wa pili.

Mafanikio yake ya haraka kwenye muziki yaliwafanya baadhi ya watu kumzushia kuwa ni mwanachama wa ‘Illuminati’, chama cha siri kinachomuabudu shetani.

Lakini watu hao wameshindwa kutambua namna msanii huyo alivyotoka mbali katika harakati zake za kutafuta maisha aliyonayo leo. Kipaji chake cha uandishi wa mashairi wenye ubunifu mkubwa, ubunifu wake katika ujasiriamali na uvumilivu ndivyo vimemfikisha hapo alipo.




Kwa uwezo wake, Octopizzo ana mustakali wa nguvu kwenye hip hop ya Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Anawaacha na fundisho vijana wanaopenda kufanya hip hop na kufanikiwa kama yeye, kuwa wanapaswa kufikiria zaidi ya kutoa ngoma na kupeleka radio. Wana uwezo wa kufikiria miradi ya kufanya na kuisaidia jamii wanayoishi kwa kujituma kuiletelea maendeleo na kuiweka kwenye ramani kwa kuitangaza kimuziki.






No comments:

Post a Comment