Sunday, June 24, 2012

Stanboi kuja na ‘Dr.Feel Good mwezi ujao



Msanii wa kimataifa wa R&B wa Tanzania aishie Marekani Stan Kibale aka Stanboi anatarajia kuachia single mpya mwezi ujao iitwayo Dr. Feel Good.

Baada ya kutoa video ya wimbo wake ‘round and round’ alikuwa amekaa kimya kidogo.

Msanii huyo ambaye yupo chini ya K-Push Entertainment mwezi uliopita alipanda stage moja na mkali wa dancehall nchini Jamaica, Sean Paul.

Kupitia mtandao wa Facebook jumatatu ya leo ameandika “fresh out of the oven,new single coming out.hope ya ready for this one.one love to all ma fans around the world,ya know i rep that 255 and all the area codes.”

No comments:

Post a Comment