Wednesday, June 20, 2012

Bi Chau:Mwanaume unarudi nyumbani mikono mitupu kama mchimba chumvi!!



Katika kusikiliza radio mbalimbali za hapa nchini kufahamu mambo gani mapya yanaendelea katika nchi yetu, tumekutana na jambo moja kubwa linalozungumzwa zaidi na magazeti pamoja na vyombo vingine vya habari.
Na lenyewe si jingine bali ni ile issue ya jana ya Mheshimiwa John Mnyika kuamriwa kutoka nje ya Bunge baada ya kuongea ndivyo sivyo. 

Bahati mbaya sisi tuna allergy na siasa labda kama ni suala lenye umuhimu wa kitaifa na maisha yetu binafsi ndo kidogo tungevumilia kusikiliza.

Basi tukapotezea na kuhamia Radio One Stereo ambako siku hizi kuna kipindi maarufu sana kiitwacho ‘Yaliyomo Yamo’. Kunongesha zaidi kipiindi hicho siku hizi huwa wanamwalika Bi.Chau na huzungumza masuala mbalimbali ya kifamilia na mahusiano. Bi. Chau anashusha madongo humooo! Tukakuta anatushushia madongo baadhi yetu wanaume.

Kuwa kuna wanaume wengine ni suruali tu. Wanaporudi nyumbani kutoka kazini ama matembezi ya kawaida hurudi mikono mitupu bila hata zawadi kwa wake zao. “Mwanaume unarudi nyumbani huna hata chungwa ama pipi ya kumletea mkeo, mwanaume gani unayerudi nyumbani mikono mitupu kama mkaanga chumvi!!” alisema Bi. Chau na kufuatiwa na vicheko vya kimbea kutoka kwa watangazaji wa kipindi hicho, si unamjua Bi. Chau alivyo na maneno mengi utadhani kameza kanda! Yeah, hata sisi tulicheka pia, very funny indeed.

“Zawadi sio lazima umnunulie nyumba ama gari, unaweza kumnunulia hata kipande cha khanga, mkeo akafurahi.” Well, alichozungumza Bi. Chau ni sahihi kabisa lakini akumbuke kuwa wanaume wengi huishia kuwahudumia wake zao kwa kuwapa mahitaji ya muhimu tu kama vile chakula kutokana na hali ngumu ya maisha ya leo.

Mwanaume anayepokea shilingi laki mbili kwa mwezi atakigawa vipi hiki kiasi kidogo anachokipata. Watoto waende shule, wavae, amvishe mkewe hata kwa matambala hayo anayoweza kumudu kununua, hata kama akiwa na uwezo wa kununua pera kama zawaidi ya mkewe, raha ya kufanya hivyo itatoka wapi?
Majukumu chungu mzima, mwanaume inabidi usali watoto wasiugue sababu mambo yatakuwa magumu zaidi. Kwa stress za maisha ya leo ni ngumu kukumbuka vitu vidogo kama hivi ambavyo kwa upande mwingine wa shilingi ni muhimu kwao wanawake.

Hakuna mwanaume anayependa kumuona mkewe akivaa nguo zile zile! Uwezo huo hana na kile anachokipata kinaishia kwenye matumizi ya muhimu tu hivyo anatakiwa kusamehewa mwanaume huyu.

Hata hivyo Bi.Chau anasema busu nalo kwenye shavu la mkeo linaweza kuwa zawadi tosha kwake ukirudi nyumbani kutoka kazini, Kweli?

Unayazungumziaje maneno hayo ya Bi. Chau?

No comments:

Post a Comment