Saturday, June 30, 2012

Zubi D'Nova: Miss India Kenya 2004 aliyekuja kuwashika kimuziki




ZUBI D'NOVA Ni nani?

Ni msaani wa Kenya ambaye kwa sasa yupo nchini Uholanzi lakini atarejea kwao Kenya hivi karibuni. Ni msanii wa kujitegemea ikimaanisha kuwa huandika na kutunga nyimbo zake mwenyewe, kufanya video zake, marketing na pia kushughulikia page zake za website na mambo mengine.

Akiwa na umri wa miaka 14, alianza kujulikana nchini Kenya kwa jina la kisanii la  ''Mellow Dee'' na kufanya collabo na wakali kama Rigga, Redsan, Vini Banton, Jaymoe, Pentamony, Syd, na wengine.

Baada ya kushinda Miss India Kenya 2004 na Zee Teen Queen - Kenya Chapter, aliendelea na muziki lakini kutumia muda wake kwenye elimu kwanza.

Baada ya kuondoa Kenya, alirejea tena nchini humo lakini muziki ukaonekana si muda wake kwa kipindi hicho na akaamua kuacha kurekodi muziki kwa karibu miaka kumi.

Na sasa Mellow Dee amerejea kwa hasira zaidi na akiwa amekua zaidi huku akija na jina jipya la Zubi d'Nova, ambalo maana yake ni ''Rise Again''.

Hii ni video ya wimbo wake mpya uitwao 'Not My Type'


No comments:

Post a Comment