Sunday, June 24, 2012

Mpenzi mpya wa Jennifer Lopez ashutumiwa kuwa ni shoga



Casper (katikati) akiwa na mashoga



Mpenzi wa Jennifer Lopez, Casper Smart ameshutumiwa kuwa yupo na mwanamuziki huyo kwasababu ya umaarufu na utajiri wake kwasababu ni shoga wa kisirisiri.

Jaji huyo wa American Idol amekuwa na uhusiano na dancer huyo kwa miezi saba sasa lakini vyanzo mbalimbali hivi karibuni vimetonya kuwa Casper ni ‘punga’ wa chini ya carpet.

Joshua Lee Ayers, dancer aliyefanya kazi na wasanii kama LL Cool J, Fergie na  Ludacris, juzi alipost picha ya Casper kwenye Twitter anayodai kuwa ni kuthibitisha kuwa Casper sio riziki.

"Check out Ur boy… And his low key homo ways," Joshua aliandika kwenye picha hiyo.

Joshua alipost picha nyingine mwezi uliopita na kuandika, “I know what I know, Not love, a lot of business and public relations."



Wawakilishi wa Jennifer na Casper wamezitupilia mbali shutuma hizo kwa kuuambia mtandao wa RadarOnline: "Casper sio shoga. Maneno haya yametokana na chuki na wivu.”

No comments:

Post a Comment