Wednesday, June 27, 2012

Diva kuandaa ziara ya kusaidia watoto yatima




Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness maarufu Diva ameandaa ziara ya kusaidia watoto waliofiwa na wazazi wao.

Kupitia mtandao wa Twitter, mtangazaji huyo amesema ziara hiyo imepewa jina la ‘Diva Giving For Charity’.

Amesema watoto hao yatima wanahitaji upendo.

Diva ameongeza kuwa leo amefanya mazungumzo na baadhi ya watu watakaodhamini ziara hiyo na tayari kampuni ya Active Finance imejitolea kumsaidia.

Hata hivyo amesema milango iko wazi kwa wale watakaopenda kumuunga mkono katika kampeni yake.

“Just incase unataka kusaidia watoto yatima katika Diva giving for charity niandikie kupitia fansofdiva@hotmail.com mwisho tarehe 15thJuly'02,” aliandika.

Hongera Diva.

No comments:

Post a Comment