Ukiwa na siku tatu leo tangu wimbo wake ‘Piga Simu’ utambulishwe rasmi na kuanza kuchezwa redioni, Diva amesema amemaliza mkataba (hopefully kusaini kabisa) wa ngoma yake kuanza kusikika kwenye makampuni ya simu.
“At cellulant life is mobile , done wit this mkataba 'piga simu will be in makampuni ya simu za mkononi very soon - happiest ever !” ametweet leo.
Kwa maana hiyo ni kuwa baada ya muda si mrefu mashabiki wake watakuwa na uwezo wa kuitumia kama ring back tone (kama mkataba huo ni kwaajili hiyo).
Sio issue kubwa sana hata hivyo kwakuwa nyimbo nyingi zipo kwenye utaratibu huo lakini kwake ni mafanikio makubwa kwakuwa wimbo hauna siku nyingi.
Huenda mkataba huo ukawa mnono sana kiasi cha kumfanya aanze kufikiria mambo makubwa zaidi, “Now I got all this shit I don't really want it..it's about the chase!!! Now I want a Bugatti! *mm*"!!!
Katika habari nyingine ni kuwa tayari amefanya mazungumzo na Adam wa Next Level ili kufanya video ya wimbo huo. “ Yay adam juma for piga simu video#fixed.”

No comments:
Post a Comment