Unamkumbuka Zay B mwanadada Gaidi? Kwa wapenzi wa Bongo Flava ya kitambo hakuna asiyemjua rapper huyu matata wa kike. Ni miongoni mwa rapper wa kike maarufu kuwahi kutokea nchini Tanzania.
Ukisikiliza wimbo kama 'Gado' akiwa na Juma Nature lazima ujiulize maswali kwanini dada huyu hasikiki tena?Uandishi wake uliwavutia wengi.
Ukiachilia mbali nyimbo za kujisifu, Zay B aliachia hits kadhaa pia za mapenzi kama “Ananitesa” aliowashirikisha akinadada ndugu wa Unique Sisters.
Tumepiga story na Zay B ambaye jina lake halisi ni Zainab kutaka kujua kwanini amepotea hivi na maisha yake yako vipi sasa hivi.
Hajabadilka sana. Bado ni msela vilevile kutokana na majibu yake lakini mwenye kuonesha uchungu mkubwa kwa namna muziki wa Tanzania ulivyokuwa leo hii.
Baada ya salamu na mambo mengine ya utangulizi swali la kwanza lilikuwa:
Leotainment: Ni muda mrefu kidogo tangu usikike, uko wapi na unafanya nini?
Zay B: Kimya changu sio kama nimeacha muziki ila niliona majungu yamezidi kwa baadhi ya wasanii,halafu likatokea tatizo lingine la kubaniwa kwenye kituo kimoja maarufu,ndo maana nikaamua nikae kimya kidogo.
Leotainment: Naamini unamaanisha Clouds Fm, lakini radio sio yenyewe,zipo nyingine pia na kuna wasanii nyimbo zao hazipigwi kwao lakini wameendelea kufanya vizuri, hebu fafanua hapo. Unapokaa kimya wengine wanahisi umeishiwa ama huwezi kwendana na muziki wa sasa!
Zay B: Wacha waamini wanavyo amini kama mtu hupewi nafasi huwezi kulazimisha mwisho unaweza kunyanyasika. Tafuta show ya Anti-virus ustawi wa jamii uone perfomance yangu ndo utapata jibu. Sasa ntafanyaje kaka yangu? Wakati watu ndo hawataki niwepo. Hua inaniuma sana navyokutana na mashabiki wangu wanavyonilaumu kwanini umeacha muziki? Wakati sijaacha, nawafariji nawaambia bado najipanga coz sio wote wanajua kinachofanyika kwenye muziki.
Leotainment: Yeah ni kweli lakini kwasababu hizo watu hawatakuelewa bado, wamekumiss sana na ulikuwa unachangamsha mno game. Wengi wanabaniwa mbona, kwanini na wewe usikomae tu? Bado una imani na antivirus?
Zay B: Najua kuna watu wamefurahi sana,na mashabiki wangu wanataka nirudi. Anti virus imesaidia baadhi ya watu wamejua ukweli.
Leotainment: Ni kweli kwamba msichana akifanya rap anaonekana malaya?
Zay B: Si kweli kama msichana akifanya rap anaonekana malaya.
Leotainment: Unauzungumziaje muziki wa sasa hivi?
Zay B: Muziki wa sasa hivi umekua, wasanii wengi wanafanya vizuri umekua kibiashara zaidi. Unajua nilivyoanza kuimba siku tegemea ntakua maarufu kuna wasanii nilikua nawapenda nikiwaona kwenye TV ndo na mimi nikatoa nyimbo hata sikutegemea nitafika mbali.
Leotainment: So unafanya nini siku hizi?
Zay B: Na dili zangu.
Leotainment: Ukisikiliza radio na unaposikia jinsi ngoma fulani zinavyopewa promo, hauumii?
Zay B: Hapana kwani kila binadamu ana nafasi yake hapa duniani na Mungu ndo anaepanga kila jambo kwa kila mtu.
Leotainment: Vp kuhusu familia? Hauna mpango wa kuolewa na kukaa nyumbani kama mke na mama watoto?
Zay B: Muda bado haujafika mimi ni mwanamke kama wengine ikifika muda nitakua mama, ila kwa sasa hivi bado na hata nikiolewa sintaacha hip hop ni hobby yangu.
Leotainment: Je! kama mumeo akikukataza?
Zay B: (anacheka) ntamtafuta anaenielewa.
Leotainment: Ulishafanya collabo na nature pamoja inspekta kipindi hicho, sasa hivi kama ikitokea ni wasanii gani wapya ungependa kufanya nao ngoma?
Zay B: Mr Blue na Ngwair naona nikifanya nao collabo tuta match kutokana na style zao na yangu inaweza ikapendeza.
Leotainment: Hujaacha tu ugaidi?
Zay B: (anacheka) kwanini unasema ugaidi sijaacha ? Huoni niko mafichoni natengeneza silaha za maangamizi?
Leotainment: Sababu bado unajiita mwanadada gaidi! Hizo silaha utazilipua lini?
Zay B: Subiri tukio ndo utajua gaidi kaibuka!
No comments:
Post a Comment