Jana 50 Cent alilazwa hospitali kutokana na kuugua tumbo ambapo rafiki yake Floyd Mayweather ambaye hata hivyo hakufafanua vizuri kuhusu ugonjwa wa swahiba wake aliwaomba mashabiki wake wamwombee.
Kwa mujibu wake Floyd, 50 Cent alikuwa mgonjwa sana.
Akionekana kwenye kitanda cha hospitali akiwa amezungukwa na midoli kibao, 50 alitweet na kusema hataki kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo mida ya saa 5:12 PM kwa saa za Afrika Mashariki (May 17) alitweet picha akiwa bado hospitali na kusema “Najiskia vizuri leo, nadhani ntatoka hospitali mapema. Jana Eminem alinipigia simu nampenda , huyo ni mwanangu”
No comments:
Post a Comment