Showing posts with label TV SHOWS STORIES. Show all posts
Showing posts with label TV SHOWS STORIES. Show all posts

Friday, August 3, 2012

D’Banj, Navio na Naeto C kutumbuiza kwenye fainali ya BBA Stargame




D’Banj ataungana na Navio wa Uganda, Khuli Chana wa Afrika Kusini, Sarkodie wa Ghana, na Naeto C wa Nigeria kwenye fainali ya Big Brother Africa Stargame.
D''Banj
Naeto C
Navio
Show hiyo ya masaa 2 na dakika 20 itaruka Live jumapili ya kesho kutwa 
August 5 kupitia Channel 198 na AfricaMagic Entertainment channel 128.


Sarkodie

Thursday, July 12, 2012

Washiriki TPF5 waishambulia Twitter kuomba kura



Mwaka huu shindano la Tusker Project Fame linaenda kidigitali zaidi. Ni mambo ya ‘twira’ tu! Thanks kwa shavu walilolipata kutoka kwa kampuni ya Sumsung ambayo imewapa washiriki simu za nguvu za Galaxy ili kujivinjari kwenye mitandao ya kijamii na kuwasiliana na mashabiki.

Leo baadhi washiriki wameutumia mtandao wa Twitter kuzungumza na mashabiki, kuahidi performance nzuri zaidi na kuomba kura pia.

Hizi ni miongoni mwa Tweets zao:

Sharon Nalwoga ‏@TPFSharon


My beloved fans am so sorry for disappointing you on last weekends #TPF5. But i promise this weekend am going to make you proud!

I would love to exchange places with Adele’s song writer. If she writes her song, then I would love to exchange places with her. #TPF5


Doreen Muchiri ‏@TPFDoreen


If I could switch places with a music idol, I would like to switch places with LAURYN HILL….maybe I will be her in the afterlife #TPF5

My #TPF5 song this week is about moving on. It's inspired by the pain & abuse of women in relationships..and infidelity too..


Steve Homes ‏@TPFSteve


Please guys vote at http://www.tuskerlager.com I want to keep on sharing this experience with you. I will not fail you…. #TPF5

The song I am writing this week is inspired by an experience in my life… I love the song too much. It is awesome!!!!!! wait for it... #TPF5

Jackson Kalimba ‏@TPFJackson




If I was to exchange places with a famous music writer it would be baby face! #TPF5

The song I’ll be singing this coming Sunday on #TPF5 was inspired by a true story that happened to me...


Nancy Bol ‏@TPFNancy



My lovely fans, please vote for me, I am asking for a favor and I promise to deliver. Please vote for me online at http://www.tuskerlager.com

Joe Irankunda ‏@TPFJoe


The inspiration of the song i'm writing this week is from a love story I had in my past so let me say that it is my past. #TPF5

East Africa, I still want to be with you & I want to sing for you, so I would like to ask you to vote for me at http://www.tuskerlager.com #TPF5

Saturday, June 23, 2012

Hakuna mtanzania tena kwenye Tusker Project Fame 5


Damian


Let’s face it! Pamoja na kuwa mashindano ya mwaka huu ya Tusker Project Fame yameongoza kwa kuwa na washiriki wabovu, wasiojua kuimba na wenye vipaji vya mashaka,Tanzania imeongoza.


Kama umepata bahati ya kuwaona watanzania walivyokuwa wanahangaika kuimba jukwaani utakuwa umejiuliza waliwezaje kupita kwenye auditions?

Wasanii wabovu kabisa! Ndo maana wametoka mapema,hakuna uonevu.

Leo mshiriki wa mwisho kutoka Tanzania, Damiani Innocent Mihayo amefungasha virago na hivyo Tanzania kutokuwa na mshiriki tena. Hiyo ina maana kuwa mashindano ya mwaka huu tutabakia kuwashuhudia tu  washiriki kutoka Uganda, Kenya, S. Sudan, Rwanda na Burundi.

Pamoja na mwaka huu shindano hili kuwa na vinono vingi kuliko mashindano yote yaliyopita kama vile kuingia kwa Samsung kusaidia masuala kadhaa ya kiteknolojia husasan simu za Samsung Galaxy, Universal Music Group nao wameingia kuweka nguvu.

Watanzania wameichezea fursa hii ya kipekee ambayo kama tungepeleka washiriki wazuri tungepata nyota mwingine mkubwa wa kimataifa.

Inauma sana!


Universal Music Group waingia mkataba na Tusker Project Fame






Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji Afrika Mashariki Tusker Project Fame msimu wa tano, limepata mchongo wa kuungana na miongoni mwa label kubwa kabisa duniani ya muziki Universal Music Group (UMG).


Hatua hiyo sasa itawaongezea nguvu zaidi washiriki wa mwaka huu katika safari ya kumsaka nyota mpya wa Afrika Mashariki.


Kutokana na ushirikiano huo, mshindi wa mwaka huu atakuwa na uhakika wa kufanikiwa zaidi kimataifa kwa kuwa chini ya usimamizi wa UMG.


Pia UMG itarekodi albam yenye nyimbo kumi ya washiriki kumi wa mwaka huu. “Wow...a whole 10 Track Album recorded by Universal Records for the Top 10 Contestants. So much at stake at ‪#TPF5‬,” imesomeka tweet kwenye ukurasa rasmi wa Tusker Lager iliyoandikwa usiku wa saa 2 (June 23) wakati show ya live ikiendelea.




UMG, ambayo lengo lake ni kufanya kazi na wasanii wenye vipaji kutoka Afrika Mashariki na kuvikuza zaidi,imebaini kuwa Tusker Project Fame ni sehemu muafaka ya kuvipata vipaji hivyo.


Mshindi wa mwaka huu atapata bahati ya kufanya kazi na kampuni hiyo iliyofanikiwa duniani na ambayo inawasimamia pia wasanii wakubwa wakiwemo Rihanna, Lady Gaga, Justin Bieber, 50 Cent, U2, Youssou N'dour na wengine wengi.

Wednesday, June 20, 2012

BBA: Prezzo aomba arudishwe kwenye eviction



Hiki kiburi cha Prezzo ni kiboko! Eti kisa hataki kumshukuru Goldie kwa kumwokoa kwenye nomination ya kutolewa, sasa anamtaka Biggie kama vipi amrudishe tu ili waafrika waamue kama watambakiza ama watamchinjia baharini.

Iangalie hapo chini.

Tuesday, June 19, 2012

Breaking News: Maneta na Roki watolewa Big Brother


Washiriki wa Zimbabwe katika shindano la Big Brother Maneta na Roki wametolewa kwenye shindano hilo baada ya kuvunja miongoni mwa sheria zake.

Wawili hao walipigana mapema leo baada ya Roki kummwagia maji  Maneta na yeye kujibu kwa kummwagia sabuni usoni na hivyo kuashiria kuwa alitaka kumdhuru.

 


Kutokana na kitendo hicho sasa wanatakiwa kupaki virago vyao na kurudi kwao kwa Mugabe.

Biggie aliwakusanya housemates kwenye lounge kuwapa taarifa hiyo fupi kuhusu uamuzi uliochukuliwa.

Maneta
Kosa hilo ndilo lililowasababishia DKB na Zainab kutimuliwa mjengoni humo wiki mbili zilizopita!

Maoni ya watu kutokana na uamuzi huo:


Charity Okon ·· Federal Polytechnic Nasarawa, Nasarawa State
This is absolute rubbish. This morning, during her dairy session, Maneta told Biggie he should not be surprised if he sees he fight, meaning she was cooking something in the offing. She sure knew she was leaving and hence decided to drag her fellow compatriot with her. This is unfair.
Reply · Like · Follow Pos
Gift Oriakhi Ajakaiye · 
OMG! Maneta knows for sure she is going and decided to take Roki with her. this years Bggie is the most messed up ever.
Liina L Amalovu · IT Department at Electoral Commission of Namibia
too bad for them......they knew the rules so they deserve it.....bt will defently miss roki he such a cool guy......en I dnt knw wts up wth maneta she have been plyin th game nicely en out of the blue acting weird......
Olaitan Habib · Obafemi awolowo univ ile ife.nigeria
FAIR! Rocki has been leading the crusade against Maneta ever since she entered the hse. Rocki knew she was angry, he kept provoking her. He just shot himself in the leg.
Adija Momoh · Federal university of technology yola
Rocki has been on Maneta's case 4 long, he is very insecure, Maneta is younger he should know better.
Vimbai Murindagomo · Northlea High School
How stupid can you get! Roki and Maneta have broken our hearts.I am very disappointed.
Adjoa Benewah Amponsah · Service Personnel at Ministry of Education
biggie shld cancel this week's nomination.
Abuya Henry · Subscribe · St. Camillus Blessed Virgins Nursery school.
this is getting freaky and freakier.
Ignatius Kadare · Zimbabwe Open University
End of the road for Zim in Biggie show.

BBA: Maneta na Roki wazichapa, hatarini kufukuzwa kama DKB na Zainab




Uwepo wa Maneta na Roki kwenye shindano la Big Brother bado upo mashakani baada ya washiriki hao kupigana na hivyo kuvunja sheria.

Kosa hilo ndilo lililowasababishia DKB na Zainab kutimuliwa mjengoni humo wiki mbili zilizopita!

Mbona hawa watu wa Upville wana matatizo sana? Big Brother ya mwaka huu mbona vizungumkuti kibao!


Sheria za Big Brother zinadai kuwa ugomvi/kupigana ndani ya nyumba unakataliwa vikali.

Big Brother, na watayarishaji wake wana haki ya kumuondoa mshiriki ambaye vitendo vyake vinakinzana na sheria za BBA.

Kwa sasa uamuzi bado haujachukuliwa kama wote watafukuzwa na tamko rasmi litatolewa baadaye.

Maneta na Roki wote ni washiriki kutoka Zimbabwe.

BBA: Uongo huu wa Prezzo waikasirisha Africa



“Kitu kizuri kuhusiana na uongo wangu ni kwamba sio uongo mkubwa ni uongo mzuri,” alisema Prezzo wakati wa mazungumzo na Big Brother. Prezzo acha zako mwanangu! Tangu lini uongo ni kitu kizuri?

Mzee huyo wa pamba alisema maneno hayo ya kujitetea baada ya Biggie kumuuliza, “Housemates ni waaminifu kiasi gani?” Kwa mujibu wa Prezzo wanawake mjengoni humo ndo wanaongoza kwa umbea. Ila kwa wanaume wote ni waaminifu kasoro Keitta.

Kinachovutia zaidi ni kuwa baadaye Big Brother alipomuuiza kuhusu uamuzi wa Goldie kumsaidia kutoka kutajwa kuondoka na kumweka mwingine badala yake, Prezzo alidanganya kuwa haoni kama ni issue kubwa. “Mi si mdadisi kiasi hicho. Udadisi ulimuua paka.” Swali ni je ni kweli Prezzo hajafurahia kuokolewa shimoni na Goldie wakati bila hivyo sasa angekuwa na tumbo joto!

Jambo la wazi kabisa ni kuwa baada ya uamuzi huo wa kuokolewa na Goldie alitoka akicheka mpaka jino la mwisho kuonekana na kuwaambia wambea wenzie Roki na Keitta: "Look at me, your boy is safe. The Head of House saved me."

Bahati ni yake ni kuwa Goldie amekufa akaoza kwake, hasikii wala haambiwi na anaendelea kuvumilia tu usela wa Prezzo wa kujifanya anamchukulia poa.
;
Soma jinsi watu walivyochukia kutokana na kauli yake:

Kay Hammer: I will kill prezzo
Kwame Danso: There's no word to describe him. Once he's on our chopping board, he's so going home
Pamela Mkosana : You can go to any other Doctor, there is no pill for stupidity....
Radebe Veronica Dieketseng :Hw stupid,shame
Thero Bradley Malebegwa :Prezzo should go home.
Ipeleng Galeboe :He is a liar,,,he shld b ashamed of himself...
Shishma Shymyeyey Jindwi: Evict him Big Brother!. Prezzo is a fool!.
Cleopatra Mahoa: Prezzo is such a smooth operator,and i dont mean it in a good way.
Amiena Goliath: Omg I dnt like this guys he thnk his all tht
Magdalene Ennin: Useless he goat an irresponsible man breakn ur wives heart on tv if I were to b his wife I wil pour hot water on hm wen he cmes home fooool
Kokeletso Koeky: Prezzo 2 the nearest exıt!!!
Lorraine Indangasi: I'm Kenyan and prezzo should come home quick!!!!!!!
Kakwete Kaitwa Musonda :Prezzo the greatest gossiper... Ummmchi

Sunday, June 17, 2012

Video: AY, MwanaFa na Sauti Sol waperform BBA



Maswahiba wawili AY na MwanaFA usiku wa kuamkia leo wameiwakilisha Tanzania kwenye Live Eviction show ya Big Brother Africa. Awali walitanguliwa na bendi ya Sauti Sol kutoka Kenya. Jionee jinsi walivyotumbuiza.


Sauti Sol


Video: Baadhi ya matukio EBSS Dodoma



Usaili wa Bongo Star Search Mjini Dodoma umemalizika Jumapili hii. Baada ya kumalizika kwake crew nzima na watu wengine ilihamia kwenye show ya pamoja ya WAKAWAKA/EBSS  hapo hapo Royal Village.

Haya ni baadhi ya matukio yaliyoendelea mjini  Dodoma.

Saturday, June 16, 2012

EATV kutoa milioni 5 kwa kundi bora la kucheza muziki



Kituo cha runinga nchini kinachosifika kwa burudani EATV kimekuja na shindano liitwalo Mia Mia Dance litakalofanyika jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo linawataka watu wenye kipaji cha kucheza kuunda kundi la watu wanne hadi sita na kwenda kwenye usaili.

Usaili unaanza Ijumaa ya tarehe 22 kwa wilaya ya Kinondoni katika viwanja vya Leaders Club.

Usaili katika wilaya ya Ilala utafanyika Jumamosi ya tarehe 23 Jumamosi kwenye viwanja vya basketball, Don Bosco, na Temeke ni Jumapili yake yaani tarehe 24 kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe.

Kundi likaloibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho litajipatia zawadi ya shilingi milioni tano.

Friday, June 15, 2012

Shocker: Prezzo anataka kuondoka BBA!



Prezzo amemuambia Biggie kuwa anataka kuondoka ndani ya mjengo wa BBA.

Katika kile kisichotegemewa, Prezzo amemwambia Biggie kuwa yeye si mfungwa na anaweza kuondoka muda wowote anaotaka na bila shaka huu ndo muda wenyewe.

Kauli hiyo iliyowashangaza wengi imetokana na Biggie kupiga marufuku matumizi ya kilevi ndani ya nyumba hiyo.

Katika kile kilichoonekana kama malumbano na Keitta, Prezzo aliomba mlango ufunguliwe ili aondoke.

Mfalme huyo wa bling wa Kenya amechukizwa na ukosefu wa mitungi mjengoni na hapendi kuambiwa na mtu yeyote kuwa hiyo ni issue ndogo na ya kupotezea tu.

Angali video hii.

Thursday, June 14, 2012

Roki alienda BBA kusafisha nyota yake ya muziki



Shindano la Big Brother Africa siku zote huwa ni jukwaa zuri kwa washiriki kutafuta exposure ya maisha yao ya baadaye. Washiriki wengi hata wale ambao hawakushinda leo hii wako sehemu nzuri na maisha yamebadilika. Wapo waliogeuka watangazaji wa radio ama TV, wapo waliopata deal za matangazo, umodel, movie nk, kutegemea na ushapu wa kila mmoja.

Hivyo kila mshiriki huenda mle kwa malengo yake binafsi. Kuna wale ambao huenda wakijua tu kwamba kupata zawadi ya mwisho si kitu rahisi lakini kile kipindi cha miezi kadhaa mjengoni huwapa umaarufu barani Afrika. Ni rahisi kufanikiwa kwa mambo yao baada ya kuwa maarufu.

Mwanamuziki wa Zimbabwe Roki anasema aliamua kwenda Big Brother ili kuongeza umaarufu wake. “Walau nikitoka nje ya nyumba hii itakuwa rahisi kwangu kumfuata msanii mwingine wa Afrika kupiga collabo kwakuwa watakuwa wameskia baadhi ya nyimbo zangu zikichezwa hapa na pia kunifahamu.Pia Napata nafasi ya kuwafahamua wasanii wengine wa Afrika.”

Lakini kwa msanii huyu, hiyo ni fursa kwake pia kuondoa mtazamo wa mashabiki kuhusu yeye kwakuwa ameharibu CV yake sana huko nyuma.Kuanzia kumshambulia mke wake mpaka kutumikia kifungo cha nje baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki bangi na mambo mengine yaliyochafua jina lake.

Pia ana watoto watano ambao kila mmoja ana mama yake. Na hao ni wale tu ambao wanafahamika.

Kwa kuonekana kwa saa 24 kwenye kamera za BBA meneja wake Bybit Areketa anasema kuwa ni nafasi ya kwake kufufuka tena kwa heshima yake na sio kama mtumiaji wa madawa, mzinzi na mpiga wanawake.

Monday, June 4, 2012

BBA: Kibao kilichowagharimu DKB na Zainab




Jana DKB wa Ghana na Zainab wa Sierra Leone wameondolewa kwenye mashindano ya mwaka huu ya Big Brother Africa baada ya kuzuka ugomvi uliomfanya DKB amtandike Zainab kibao kikali.

Angalia jinsi ilivyokuwa.



Unadhani chance ya Prezzo kuzikamata $300,000 umeongezeka?

Saturday, June 2, 2012

Goldie agoma kula, ahofiwa kutaka kujiua kisa Prezzo

Siku za hivi karibuni Goldie wa Nigeria amekuwa akikataa kula chakula huku wenzake kwenye jumba la BBA wakihofia kuwa huenda akajaribu kujiua.

Habari hizi zimewekwa wazi na Maneta wakati wa mazungumzo na Prezzo ambaye alishusha bomu jingine kuwa Goldie si dem wake.

Hayo yote yamekuja baada ya uhusiano kati ya Goldie na Prezzo kuingiwa na mdudu mbaya aliyeuchachua utamu wa penzi changa lililokuwa limeanza kuota kwenye udongo wenye rutuba.

Prezzo sasa hivi anaonekana kumfukuzia Zainab. Kwa mujibu wa Maneta, Goldie anaonesha dalili za kujiua na amekuwa akionesha tabia za ajabu tangu Prezzo ampige chini.

"Msichana huyu atajiua. Hataki kula na kusingizia anaumwa jino," Maneta alisema.

 ‘Amekuwa akijigeuzageuza kitandani na kuoneshaa vituko. Nadhani anataka attention pia,” Maneta aliendelea.

Prezzo alikuwa akisikiliza kwa makini wakati mwakilishi huyo wa Zimbabwe alipokuwa akimpa muhtasari wa kinachoendelea.



Kutokana na kuzinguana kwa Goldie na Prezzo baadhi ya watu wameanza kumtupia lawama Zainab kuwa ndio chanzo.

Friday, May 25, 2012

Trouble in Paradise: Prezzo na Goldie wazinguana



Baada ya siku kadhaa za mahaba mazito kati ya Prezzo na Goldie, hatimaye ibilisi ameingia katikati yao na sasa 'the party is over and here comes trouble'!

Mtoto Goldie anamind eti Prezzo anamchukulia poa!

"Unadhani mimi ni mto wa kochi, kuwa real kwako mwenyewe,” Prezzo alisema. Goldie akabaki mdomo wazi na akashindwa kuamini kama maneno hayo yametoka kwa Prezzo mwandani wake ama mtu mwingine.

Lakini Prezzo hakuishia hapo, akamwongezea mrembo huyo dongo jingine"Do you have a goldfish memory? I'm not a kid so don't treat me like one,"! Duu!  

Prezzo analalamika kuwa wote wamekuwa wakiendelea kujitahidi kuweka maisha yao safi mjengoni lakini sasa mambo yanaanza kumshinda.

Monday, May 21, 2012

Hilda, Julio na Teclar wazungumzia wiki moja ya BBA



Baada ya kutolewa katika wiki ya kwanza tu ndani ya Big Brother Africa, waliokuwa wawakishi wa Tanzania Hilda na Julio pamoja na Teclar wa  Zimbabwe wameelezea namna wiki moja ilivyokuwa kwao.


\

Sunday, May 20, 2012

BBA: Watatu watoka, Camp Mulla waacha gumzo Afrika Kusini



Jana ilikuwa siku ya eviction ambapo wawakiilishi watatu walitoka ambao ni Dalphin wa Sierra Leone na waLiberia Yadel na Luke huku Zainab wa Sierra Leone akihamia Upville.

Lakini kilichovutia zaidi ni show iliyopigwa na vijana  watano wa kundi la Camp Mulla la nchini Kenya na ngoma yao Fresh all day. Waangalie  jinsi walivyoshangiliwa.

BBA: Prezzo na Goldie ndani ya penzi zito



Inaonekana penzi kati ya Prezzo na Goldie linaendelea kushamiri.
Mchana wa jana mastaa hao walikuwa wamegandana kama gundi.
Muda wote walikuwa pamoja utadhani hakuna washiriki wengine ndani ya jumba hilo. Mara nyingi wameokana wakiwa kwenye kochi wakicheka , wakilaliana na kushikana mara kwa mara.

Roki alijaribu kuungana nao katika mazungumzo lakini wakampotezea hivyo kujiondokea na kutafuta jambo la kufanya na kuwaacha wapenzi hao kwenye mahaba mazito.



Barbz: Wananielewa vibaya

Katika hatua nyingine Barbz amekaa na DKB kuzungumza yaliyomo moyoni mwake kuhusiana na jinsi watu wanavyomuelewa vibaya na ndo maana akaamua kushiriki BBA ili watu wamfahamu vizuri lakini hata hivyo ndani ya jumba hilo bado wanamchukulia tofauti, jambo linalomuumiza sana.




Ni kubanjuka tu


Upande wa Upville baadaye pakageuka club ya disco. Ukapigwa muziki mtamu na washiriki wakasakata rhumba. Hata hivyo akinadada ndio waliojituma kucheza zaidi.

                  


Ukizingua, nazingua pia


Huko Downville mambo si mambo. Keagun(Afrika Kusini)  na Junia (Namibia) wakajikuta kwenye vita kali ya maneno.