Sunday, June 17, 2012

Makala: Father's Day ilianzishwa na Mwanamke


Sonora Dodd

Leo ni Father’s Day na bila shaka ulitaka kujua ilianzaje. Father's Day ni sherehe ya kuwaenzi akina baba na kusherehekea ubaba, uzazi na mchango wa akina baba kwenye jamii.

Nchi nyingi hushereheka siku hii kila jumapili ya tatu ya mwezi June lakini husherehekiwa pia katika siku zingine kutokana na uamuzi wa nchi husika.
Baada ya mafanikio yaliyopatikana na Anna Jarvis kutokana na kuipigia debe Mother's Day nchini Marekani, baadhi ya watu walitaka kuunda siku nyingine kwa ajili ya member wengine wa familia na chaguo la Father's Day likaonekana kufanikiwa.

Lil Wayne na mwanae
Kulikuwepo na watu wengine nchini humo ambao walipigania binafsi kuwepo kwa "Father's Day" lakini sifa kwa siku hii leo zinapelekwa kwa Sonora Dodd.
Father's Day ilianzishwa mwaka 1910 na Sonora Smart Dodd (Mwanamke) aliyezaliwa huko Arkansas.

Sherehe ya kwanza ilifanyika Spokane, Washington June 19, 1910. Baba yake aliyekuwa mstaafu wa jeshi William Jackson Smart, alikuwa ni mzazi aishiye bila mke na ambaye alikuwa na watoto sita huko Spokane, Washington.
Baada ya kusikia hotuba ya Jarvis kuhusu Mother's Day mwaka 1909, alimwambia mchungaji wa kanisa alilolokuwa akisali kuwa akina baba wanapaswa kuwa na siku yao kama hiyo ili kuwaenzi.

Mpiga picha maarufu nchini, Raqey Mohamed
Ingawa alipendekeza kuwa June 5, iliyokuwa siku ya kuzaliwa ya baba yake, wachungaji hawakuwa na muda wa kutosha kuandaa ya kuzungumza hivyo ilibidi waipeleke hadi wiki ya tatu ya mwezi June.

Siku hii haikuwa na mafanikio  mwanzo. Miaka ya 1920s, Dodd aliacha kupromote sherehe hiyo kwakuwa alikuwa anasoma chuo cha Art Institute of Chicago, na siku hiyo kupoteza umuhimu wake.

Miaka ya 1930s Dodd alirejea Spokane na kuanza kuipromote tena siku hiyo kwa kuongeza ufahamu wake kwenye ngazi ya kitaifa.

Tangu mwaka 1938 alipata msaada kutoka kwa baraza la Father's Day lililoanzishwa na New York Associated Men's Wear Retailers kuimarisha promotion ya siku hiyo kwa mfumo mzuri zaidi na wa kibiashara.

Wamarekani waliipinga sherehe hiyo kwa miongo kadhaa sababu waliiona kama njia ya wafanyabiashara kuiga umaarufu wa Mother's Day, na magazeti yalikuwa yakiandaa habari za kuishambulia kwa utani mwingi.

JCB na Mwanae
Hata hivyo kundi hilo halikukataa tamaa. Liliendelea kuipigia debe na hata kutumia utani uliotumiwa kwenye matangazo na hatimaye walifanikiwa.
Muswada juu ya utambuzi rasmi wa sherehe hiyo ulitambulishwa kwenye bunge la Congress mwaka 1913.  

Mwaka 1916, rais wa Marekani wa kipindi hicho Woodrow Wilson alienda mjini Spokane kuzungumza kwenye sherehe za Father's Day na kutaka kuifanya iwe rasmi lakini bunge la Congress lilipinga kwa kuhofia kuwa siku hiyo itafanywa kuwa ya kibiashara.

Jay-Z na binti yake Blue Ivy
Rais Calvin Coolidge mwaka 1924 alipendekeza kuwa siku hiyo inapaswa kutambulika kitaifa lakini alisita kutoa tamko la kitaifa.

Mwaka 1966, rais Lyndon B. Johnson alitoa tamko la kwanza la rais kuhusu kuitambua rasmi siku hiyo na kwamba itakuwa ikifanyika kila wiki ya tatu ya Jumapili katika mwezi June.

Miaka sita baadaye siku hiyo ikafanywa kuwa ya sikukuu ya kitaifa pale rais Richard Nixon aliposaini sheria hiyo mwaka 1972.

No comments:

Post a Comment