Showing posts with label OTHERS. Show all posts
Showing posts with label OTHERS. Show all posts

Sunday, August 19, 2012

Ujumbe wa Eid kutoka Leotainment



Tunayo furaha kuungana na waislam wote duniani katika sikukuu hii muhimu ya Eid El Fitr. Kwetu sisi tunaichukulia kama siku ya ushindi kwa waislam wote waliotumia siku 30 na ushee katika mfungo wa mwezi wa Ramadhan kwa kujinyima na kujitesa ili kukamilisha nguzo muhimu ya uislam. 

Tungependa kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru waislam wote na wale wasio waislam kwa kutuunga mkono katika blog yetu. Pamoja na uchanga wake na ikiwa na miezi minne tu, Leotainment imekuwa miongoni wa blog zinazosomwa na wapenzi wa habari za burudani kwa wingi zaidi. 

Imekuwa chanzo cha habari kwa blog na website zingine nyingi ndani na nje kitu ambacho kamwe kisingewezekana pasipo ushirikiano kutoka wasomaji waaminifu wanaotuunga mkono siku zote. 

Ombi letu kwenu ni kuendelea kutuunga mkono bila kuchoka na pia kuwaambia marafiki na watu wa karibu kuhusu uwepo wetu. Tunaahidi kuendelea kuwa blog inayoandika habari za burudani kwa umakini na kuzingatia sheria zote za uandishi wa habari huku tukiendelea kukupasha kwa habari mpya muda wote.

Tunawatakia sikukuu njema yenye amani. Eid Mubarak.

Timu ya Leotainment.

Saturday, August 18, 2012

Nape: mataifa ya nje yameweka vibaraka kuvuruga siasa ya Tanzania



Jumamosi katika kipindi cha Makutano ndani ya Magic FM katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye aliongea kuhusu kauli yake kuwa Harambee za CHADEMA ni za kisanii kwani kuna wafadhili ambao wako nje ya nchi wanaotumia mwanya huo kukifadhili chama hicho.

Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimkaribisha katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye kwenye studio za Magic FM
Nape alisema kuwa kuna hela chafu zinazoingizwa na Mataifa yanayotaka kuvuruga siasa na kuwaweka vibaraka ambao watafanya kile wanachotaka  watu hao wanaozimezea mate rasilimali za nchi husika huku akitolea mfano wa Congo.
Nape Nnauye katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango, Musa Kipanya na Mwanasheria Joseph alieelezea sheria za msajili wa vyama vya siasa.
Aliendelea kusema kuwa kuna pesa chafu ambazo zinaingizwa toka nje na kuchangiwa katika harambee na watu wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa. Nape amewataka chadema kutoa majina ya watu waliowachangia na kazi wanazozifanya ili jamii iwatambue. 

Alipoulizwa kama anayafahamu majina ya wafadhili wa nje wa chadema kwa nini asiyataje Nape alijibu katika siasa kuna kitu kinaitwa “Timing” kwamba anasubiria wakati muafaka huku akitolea mfano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alieitaka Serikali iwataje vigogo wanaomiliki mabilioni katika mabenki ya nje ya nchi la sivyo atawataja. 

Alimaliza kwa kutaka kila mtu ahakikishe anapigania amani ya nchi.

Friday, August 17, 2012

TBC yawaomba radhi waislam kwa kutoa takwimu zisizo sahihi

Mkurugenzi Mkuu wa TBC Clement Mshana

Shirika la utangazaji Tanzania, TBC, leo limewaomba radhi waislam nchini kwa kutoa takwimu zisizo sahihi za waislam na wakristu.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Clement Mshana amefafanua kupitia kipindi cha Jambo Tanzania leo asubuhi kwa kukiri kuwa mmoja wa watangazaji wa TBC1 alitaja takwimu za  wakristu kuwa ni asilimia 52% na waislam asilimia 32% zilizopatikana kutoka mtandao wa Wikipedia.

TBC imeomba radhi kwa kuwapotosha watanzania kwakuwa takwimu hizo sio sahihi.

Mshana alikiri kuwa TBC ilifanya kosa kuunukuu mtandao wa Wikipedia na kudai kuwa chombo chenye mamlaka na cha kuaminika ni  Wakala wa Takwimu nchini na sio wikipedia.

Mkurugenzi huyo amesema tarehe 15, May, 2012 shirika hilo liliandika barua ya kuomba radhi kwa jumuiya ya waislamu nchini na kumpa onyo mtangazaji aliyetaja takwimu hizo.

Ametaka waislam kusahau yaliyopita na kuutumia mwezi huu wa Ramadhan kusamehe huku akiwataka wananchi kujitokeza zaidi kwenye zoezi la sensa litakalosaidia kupatikana kwa takwimu sahihi.

Saturday, August 11, 2012

Exclusive: Makala ya kusisimua kuhusiana na maisha magumu ya mdogo wake Obama



Obama's slumdog brother: Kutana na mlevi asiye na matumaini aishie jijini Nairobi ambaye ni mdogo wake na rais wa Marekani

Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye gazeti la Daily Mail mwandishi akiwa  ANDREW MALONE. Makala hii imechapishwa jana, August 10, 2012.

Wakati mwanaume mrefu na anayejulikana sana akiondoka kwenye kibanda chake kilichopo kwenye makazi fukara kabisa barani Afrika wiki hii, baadhi ya watu walianza kumuita kwa utani:‘Mister President! Mister President!’

Akielekea kupata kifungua kinywa huku akivuka mifereji inayotiririsha maji machafu, muonekano wa jamaa huyu mrefu na aliyekonda, unavutia vicheko vya chini chini kutoka kwa watoto wanaocheza kwenye jalala.
George akiwa kwenye nyumba anayoishi
Jina la jamaa huyu ni George Hussein Obama, ni mdogo wake na Barack Hussein Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani na mwanaume anayeheshimika zaidi duniani.


Wanaume hawa wawili wanachangia baba lakini Barack Obama alizaliwa Hawaii kwa mke wa pili wa baba yao ambaye ni mmarekani na George alizaliwa nchini Kenya akiwa mtoto wa mke wanne wa mzee huyo.

Leo, wakati Barack akifurahia maisha kwenye Ikulu ya White House, akiruka kwenda nje na Air Force One na ni rafiki wa mastaa wa filamu na wengine mashuhuri, George, 30, anapatikana akiwa amechoka kwenye makazi yake ambayo hata wakazi wenzake wa eneo hilo maskini jijini Nairobi wanayaona kama kichuguu.


Ingawa anadai kutotumia heroin au cocaine, George hutumia muda mwingi kunywa Gongo (Chang’aa) kuanzia anapoamka mpaka muda ambao huanguka na kuzima kabisa.

Gongo anayokunywa ni ile iliyochanganywa na kemikali ya ethanol, na kuongezea acid kutoka kwenye betri ili kuipa kick zaidi, na mchanganyiko huu husababisha upofu na kifo inapochanganywa vibaya.

Kiasi kidogo tu cha pombe hiyo huwafanya hata wanywaji wazoefu kulewa kiasi cha kushindwa hata kukumbuka majina yao. Wanywaji wa mara kwa mara huathrika maini na figo ama ubongo.


Nilipomtafuta George asubuhi siku moja kufahamu maisha yake, alikuwa tayari kwenye kibanda kimoja jirani akinywa Chang’aa ambapo ngono na machangudoa ni sehemu ya menu na hufanyika kwenye kitanda kilichowekwa nyuma.

Utambulisho unafanywa na ‘mpambe’ wa George  — mkazi wa eneo hilo mwenye macho mekundu na mnywaji mwenzie ambaye anamvuta George nje ya kibanda hicho na kumwabia aje kumuona mzungu nje (shouting at him to come and see the ‘muzungu’ (white man) outside.

Baadaye baada ya kusalimia, ninafanya kosa. Namkaribisha George kwaajili ya chakula cha mchana kwenye hoteli yangu. Kwa siku mbili zilizofuatia, aliivamia baa yangu ndogo, kuwaalika wapenzi wake kibao na washkaji zake kula na kunywa kwa gharama zangu na kujionesha kama staa aliyeharibikiwa.

Aliomba pia ‘kitu kidogo’ — Swahili for something small, which, of course, means something large and financial — na alichukia baada ya mimi kukataa kuwapa hela mademu zake.

George pia aliendelea kulaumu kuhusu jina la Obama kuwa kama mzigo na laana kwake, ilhali wakati mwingine bila aibu hulitumia jina hilo kupata hela nyingi iwezekanavyo ili kuzitumia kunywa na kuvuta bangi.

‘Watu wanavutiwa na mimi kwasababu ya kaka yangu,’ anashusha pumzi na kushusha  Johnnie Walker mbili kwa mpigo. ‘Nachukia’. Watu wanapenda niwe mtu mwingine.’

Mara ya kwanza George alikutana na kaka yake alipokuwa shule ya msingi. Barack alienda Nairobi miake michache tu baada ya baba yao kufariki kwa ajali ya gari. George anakumbuka alikuwa akicheza soka wakati kaka yake alipowasili kumsalimia.

Mara ya pili wanakutana ni kipindi Obama — alipokuwa Senator na alifanya ziara ya Afrika Mashariki mwaka 2006, na kutembelea Nairobi kuiona familia yake.

George anasema kwa sasa watu wanamshinikiza afuate nyayo za kaka yake kwenye siasa. ‘Nina watu wengi ambao huniambia nigombee ubunge. Lakini sivutiwi na siasa.’

Kisha anatulia, na kuongeza: ‘Lakini kama Barack angekuwa rais na mimi ningekuwa rais wa Kenya ingekuwa rahisi kuonana.’

Anasema umaskini wake ndio unawazuia ndugu hao kuwa na uhusiano wa karibu.

‘Ana majukumu. Hatakiwi kunilea mimi,’ anasema. Mimi ni mtu mzima, kila mtu hudhani kuwa huwa ananitumia fedha. Lakini mimi sio ombaomba.’ Lakini alipoulizwa iwapo aatachukua fedha akipewa na Obama alisema: ‘Seriously! Yes! Who wouldn’t?’

George alikulia jijini Nairobi akiwa na mama yake ambaye aliolewa tena na mfaransa aliyekuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada jambo ambalo anadai lilimfanya awe hivyo.

Alianza kunywa pombe na kuvuta bangi akiwa na miaka kumi, miaka mitano baadaye alifukuzwa kwenye shule ya boarding, ambako alicheza rugby na kujifunza lugha za kigeni kutokana na kutumia madawa ya kulevya.

Anakubali kuwa alikuja kuwa addicted na cocaine na heroin akiwa na miaka 17, na kuwa mwizi wa kutumia silaha ili kupata hela ya kunywea pombe.

Mwaka 2003 alifungwa jela kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha.

Alikaa kwa miezi tisa kabla ya kutoka kutokana na kukosekana ushahidi.

Swali ni je! George anastahili kuishi maisha haya wakati kaka yake ni rais wa Marekani?

Monday, July 30, 2012

Tuhuma za rushwa:Zitto Kabwe kuzungumza na waandishi kesho



“Kesho Nitazungumza na waandishi wa Habari ofisi za Bunge Dar Es Salaam kuanzia saa tano asubuhi. Kuendelea kukaa kimya ni silaha kwa adui,” ametweet Zitto jioni hii (July 30).

“Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu.
Nimetaka chama changu kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi.”

Tuesday, July 24, 2012

Miss World yaongeza shindano la kura za Facebook! Lisa Jensen anahitaji kura zenu

Miss Tanzania 2012 Lisa Jensen

Miss World 2012 imekuja na shindano jipya liitwalo  “People's Choice Online Voting” linaloruhsu wananchi kuwapigia kura washiriki wawapendao kwa kulike page zao za Facebook.

Kwenye shindano hilo kila mshiriki atatumia ukurasa wake wa Facebook kushare taarifa zake mwenyewe na kuitambulisha nchi yake, icha zake, video pamoja na habari za trip yao inayoendelea ya China.

“People's Choice Online Voting” itaendela hadi August 15, siku tatu kabla ya fainali.

Hizi baadhi ya video za utambulisho wa washiriki hao.

1. Miss World Tanzania




















Wednesday, July 18, 2012

Vyanzo: Ndege ya ATCL Yapasuka Kioo angani; yazuiwa kuruka KIA



Habari za uhakika zinadai kuwa ndege ya ATCL namba TC 100 ambayo ilikuwa imeondoka Dar mapema asubuhi ya leo (July 18) kuelekea Mwanza ikipitia KIA imepasuka kioo.

Taarifa zimedai kuwa kioo hicho kilipasuka wakati ndege hiyo ikijiandaa kwenda Mwanza baada ya kuwa imeshatua KIA.

Kioo kilichopasuka ni kile cha pembeni kwa rubani upande wa kushoto kwa mujibu wa vyanzo.

Kutokana na tukio hilo ndege hiyo ilizuiwa kuruka hadi pale marekebisho ya kioo hicho yangefanyika.

Haijajulikana iwapo imesharuhusiwa ama bado.

Source: Jamii Forums.

Saturday, July 14, 2012

Wednesday, July 11, 2012

Video: Mdogo wake Barack Obama bado choka mbaya



Mdogo wake na rais wa Barack Obama wa Marekani, George Obama bado ameendelea kuishi maisha magumu kwenye nyumba ya matope (slum) nchini Kenya.

“Nadhani ana familia yake mwenyewe,” alisema George Obama katika mahojiano na mwandishi Dinesh D’Souza.

“Mimi ni member wa familia yake lakini nina umri mkubwa, hivyo najisaidia mwenyewe,” mdogo wake na Obama alisema kwenye clip hiyo ya dakika nne iliyopo kwenye website ya Hollywood Reporter (www.hollywoodreporter.com).

D’Souza, mwandishi wa kitabu cha mwaka 2011 kilichouza sana “The Roots of Obama’s Rage,” alisema alimtafuta mdogo wake na Obama baada kumuona kwenye habari iliyomwonesha akiishi kwenye kijibanda jijini Nairobi.

Alipoulizwa na mwandishi huyo iwapo kaka yake ameshindwa kumsaidia George Obama alijibu: “Ana mambo mengine ya kushughulikia.”


“He’s taking care of the world, so he’s taking care of me.”

Singita Grumeti Reserves ya Serengeti yawa hoteli bora duniani 2012


Singita Grumeti Reserves
Tujilaumu wenyewe kwa kutofanya utalii wa ndani kiasi cha kushindwa kujua kuwa hoteli bora kabisa duniani inapatikana kwenye ardhi ya Tanzania. Habari ndio hiyo, hoteli bora duniani ipo Bongo!

Kwa mujibu wa matokeo yaliyopatikana kutokana na survey inayofanywa kila mwaka na jarida la Travel + Leisure kwa mwaka wa pili sasa, Singita Grumeti Reserves inayopatikana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti, nchini Tanzania, ndio hoteli bora kuliko zote duniani! 

Ni cheo kikubwa kikitajwa kwako na hasa ukizingatia jinsi unavyoijua nchi yako lakini kumbuka kule Serengeti ni duniani nyingine kabisa, hivyo usishangae kwakuwa watu wamewekeza hasa! Watu wanakula bata kule!

Hoteli hiyo imescore asilimia 98.25 na kuifanya kuwa ya kwanza duniani.

Ona jinsi Tanzania ilivyobarikiwa!
Ukiwa chumbani unaweza kuona wanyama kwa nje

Kura hizo zimepigwa na wasomaji wa T+L ambao ni wapenzi wa kusafiri duniani kula bata na kusema ni hoteli gani wanazipenda zaidi. 

Vigezo vya kuchagua hoteli bora vinaanzia kwenye vyumba vyenyewe, eneo ilipo, huduma inayotolewa pale, chakula na thamani.


Msosi unapigwa hapa
Ukitaka jakuzi la aina hii, ni chaguo lako tu

Ukitaka kuzijua hoteli zingine bora duniani click hapo chini.


Maelezo ziadi kuhusu Singita Grumeti Reserves

The Singita Grumeti Reserves  (Best Hotel in the World 2011) offers an unparalleled eco-safari teeming with magnificent wildlife encounters on the western corridor of the Serengeti. This vast private concession comprises an exclusive trio of luxury lodges positioned ideally on the epic migratory route traversed annually by more than a million wildebeest. If it is solitude you seek then Singita Grumeti Reserves is the place to be.


The area is home to large herds of game that provide world-class photo opportunities all year round. Each of the lodges offer a unique experience: Singita Sasakwa Lodge positioned on Sasakwa Hill, presents dramatic, elevated views across the endless plains, Sabora Tented Camp celebrates flat open space as far as the eye can see and Faru Faru Lodge is tucked away in a diverse habitat.

The price per night per person ranges from US$1,700 sharing. The price Includes: Luxurious all-suite accommodation, breakfast, lunch and dinner daily, teas and coffees, two open Land Rover safaris a day accompanied by experienced guides. All drinks, including wines, spirits and liqueurs (excluding French champagne) .Return surface transfers from the Sasakwa airstrip to the lodges and Government of Tanzania Wildlife Fees of US$50 per person per night.

Valuetrip gives 5 starts in comfort in the middle of the jungle, services, Its incredible location, atmosphere, activities and for the Safari adrenaline.

Tuesday, July 10, 2012

Wazazi washikiliwa na polisi wa UAE kwa kumweka mtoto kwenye begi



Wanandoa wa nchini Misri wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumweka kwenye begi la nguo ili wawapite walinzi wa airport huko katika Umoja wa Falme za kiarabu (UAE).

Walinzi hao walimkuta mtoto huyo mwenye miezi mitano kwenye begi hilo dogo la nguo.

Polisi wamesema mtoto huyo aligunduluwa kwa X-ray kwenye uwanja huo wa ndege wa  Sharjah International Airport wakati wazazi wake walipokuwa wakisubiria kusafiri.



Hata hivyo mtoto huyo anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa polisi wa Sharjah, wanandoa hao waliwasili UAE ijumaa iliyopita lakini walizuiwa kuingia nchini humo kwasababu hawakuwa na visa ya mtoto wao.

Wazazi hao waliambiwa kusubiri kwa siku mbili hapo airport mpaka ofisi ya visa itakapofunguliwa ili visa ya mtoto wao iwezi kushughulikiwa.



Siku ya jumamosi baada ya uvumilivu kumshinda, baba wa mtoto huyo alimshawishi mke wake wamweke mtoto wao kwenye begi akiamini kuwa security hawatamuona.

"Tulishangaa sana. Hii ni mara ya kwanza kuona kitu kama hivi,” afisa wa polisi Abdel Rahman Shama aliiambia CNN. "Hata kama umekataa tamaa, utamwekaje mtoto kwenye begi?’

Wazazi hao wanashikiliwa na polisi nchini humo.

Saturday, July 7, 2012

Maajabu: Hela za sadaka zageuka makaratasi





Wanasema maajabu kamwe hayataisha. Huko Nigeria kwenye parokia ya St. Mary's mjini Jos, Plateau State, wameshangazwa baada ya kupotea kimauzauza naira 300,000 (sawa na karibu shilingi milioni 3) zilizobadilika kimaajabu na kuwa makaratasi.

Vyanzo vya nchini Nigeria vimedai kuwa tukio hilo la ajabu limetokea kwenye benki ya  Zenith tawi la Jos, ambapo katibu wa kanisa Miss Ifeoma Eze alikuwa ameenda kuziweka benki fedha hizo za sadaka kwa siku hiyo.

Ifeoma alieleza kuwa pesa hizo zilikuwa salama alipoondoka nyumbani kuelekea benki lakini alipofika kwenye kaunta ya benki hiyo hakuelewa ni kwa namna gani fedha hizo ziligeuka na kuwa vipande vya karatasi alipofungua mfuko alimokuwa ameziweka.

Alichanganyiwa na kuogopa kiasi cha kumfanya aanze kupiga mayowe (kama wale wanawake kwenye movie za kinaijeria) ambapo wateja wengine walimzunguka kumuuliza kunani!

Miss Ifeoma alisema alikuwa amechanganyikiwa zaidi kwakuwa alijiuliza angemweleza nini padre aliyemkabidhi fedha hizo!

"Ni habari ambayo inakuwa vigumu kumweleza mtu sababu wengi hawataanini,” alisema.

Kudhihirisha kuwa alichukua fedha za kweli kwenda benkini hapo, Miss Ifeoma alisema kwanza alibadilisha chenchi ndogo ndogo na kuchukua kubwa ili kurahisisha uwekaji.

Ingawa waamini wa kanisa hilo wanahisi kuna mchezo mchafu umefanyika, Askofu wa parokia hiyo Father Emmanuel Ray-Ikpe, amelielezea tukio hilo kama la bahati mbaya, la kushangaza na ajabu.

"Sijawahi kusikia kitu kama hicho kabla, lakini kimetokea kwetu, kanisani kwetu. Hatuna cha kufanya. Katibu wangu alikuja kutoka benki akilia. Mungu ndo anajua nini hasa kimetokea. Tumeyaacha yote kwenye mikono ya Mungu muumba wetu," alisema askofu huyo.
.

Wednesday, July 4, 2012

Leotainment's Picture of the day


Picha kumi zinazochekesha zaidi Facebook 2011-2012

Katika pitapita zako Facebook bila shaka ulishakutana na picha hizi kumi. Ni picha maarufu sana kwenye  mtandao huo wa kijamii na mara nyingi bado zinaendelea kuonekana kutokana na watu kuzishare.


Picha zenyewe ndo hizi.


1. Jamaa aliyeamua kupunguza 'upwilu' kwa kufanya mapenzi na mbuzi! What a shame!
2.Afande Sele alipoamua kubaki na kiboxer tu
3.Maustaadh hawa walipoamua kung'oana jino kibabylon
4. Asiyefanya kazi na asile
5. Hii ndo hali halisi
6. Kibonde the birthday bway!
7. Loser to pay, winner to stay ndo mpango
8.Nichumu mwaaaaaa!
9. Radio inapomeza kanda
10. Vp! Msosi bado tu?

Tuesday, July 3, 2012

Facebook yaongeza icon ya mashoga kwenye timeline



Baada ya mmoja wa waanzilishi wa Facebook Chris Hughes ‘kuolewa na mpenzi wake wa siku nyingi  Sean Eldridge huko New York City, Marekani, jumamosi iliyopita, mtandao huo maarufu wa kijamii umeamua kuanzisha alama ya kuonesha status kwa wapenzi wa jinsia moja.

Chris Hughes (Kushoto) na Sean Eldridge walipofunga ndoa jumamosi
Kwa kawaida wakati watu wanapobadilisha status kutoka single, engaged ama it’s complicated na kwenda 'married' kulikuwa na kiicon cha mwanaume akiwa na mwanamke kwenye timeline, lakini sasa hivi kuna alama imeongezeka ya mwanamke akiwa na mwanamke ama mwanaume akiwa na mwanaume.

Facebook banaaaaa!