Wiki hii rapper wa Tanzania aliyepo nchini Sweden ameachia bonge la video ya wimbo wake uitwao Pretty Girl aliomshirikisha Obi Elinami.
Leotainment imetaka kujua zaidi kuhusiana na video hiyo na kuamua kumtafuta na kuzungumza machache kama ifuatavyo:
Leotainment: Umetoa video kali sana. Mpaka video imekamilika umetumia kama shilingi ngapi za haraka haraka?
Janb: Imenitoka US dollar 13,500 mfukoni (Takriban mil.20). Japokuwa/ila gharama nyingine director wa video alinisaidia kwa kuwa aliniona niko serious katika game na ndo kwanza naanza na sina kitu.
Leotainment: Mlitumia siku ngapi kushoot?
Janb: Tulitumia siku mbili (2) siku ya kwanza ilikuwa footage za studio siku ya pili footage za ndani(mjengoni) siku ya kwanza tulitumia masaa 9 na siku ya pili masaa 5.
Leotainment: Kama umeshawahi kushuhudia shooting ya video za Bongo, hao jamaa wanafanya kitu gani katika shooting ambacho huku hakifanyiki?
Janb: Kiukweli siwezi kabisa kufananisha hawa jamaa au huyu jamaa (Duncan Mukada) na kampuni yeyote ile Tanzania, East Africa na Africa ikibidi. Jamaa ni professional for real. Wako professional kuanzia script writing..maake lazima video scene ziendane na wimbo wenyewe, namaanisha kwamba hata mtu yeyote anayeangalia music video hata kama haelewi lugha ila anaweza kuangalia scenes na akapata picha kamili.
Pia kuhusu editing jamaa wako next level wanafanya editing professionally. Kwenye shooting wanakuwa kama team player, kila kitu kinafanyika according to scripts na team ya ma producer wako fit katika kuandaa msanii/wasanii wakati wa video shooting, i mean kuanzia mavazi, appearance, na muonekano katika video.
Leotainment: Umewapata wapi hao mamodel? ni wa nchi gani na majina yao?
Janb: Mamodel alinisaidia director wangu maake keshafanya video nyingi na wasanii wakubwa hapa Sweden. Aliniunganisha nao then nikaongea nao tukakubaliana deal ya kufanya nao kazi, na huyo model ambaye ni main character ni miss Africa crown scandinavia 2011/2012...ni maarufu sana hapa Sweden and super model.
Leotaiment: Umeshaituma kwa vituo vya runinga vya Bongo?
Janb: Yes, karibia vituo vyote vikubwa na vidogo vya TV Bongo/Tanzania nimewatumia video yangu,pamoja na radio stations nimewapatia audio. Pia nimetuma video yangu katika DSTV channel za Trace urban, Channel O na Mtv Africa ila wiki hii ndo natuma pia broadcasting contract ambayo nilijisahau kuituma,na bila hiyo contract hizo channel hazichezi video yako!
Pia good news ni kwamba nimepewa nafasi kupata VEVO account kupitia distributor wangu anayeuza nyimbo zangu katika online store, so, kuanzia mwezi ujao ntakuwa na original VEVO account kama wasanii wengine wakubwa duniani, ambacho hakijawai kutokea kwa msanii yeyote wa Africa Mashariki.
Leotainment: Baada ya video ya Pretty Girl nini kipya kutoka kwako kinachokuja?
Janb: Watanzania na mashabki wangu wategemee mambo makubwa kutoka kwangu katika tasnia ya muziki, niko nafanya mixtape yangu inayoitwa 'Swahili swag'' itatoka mwaka huu. Pia natarajia kufanya video nyingine ambayo itakuwa level nyingine kabisa ''Big budget video'' ila sijaamua nyimbo gani nifanyie video mpaka leo hii ila mpaka mwezi ujao ntakuwa nshafanya decision kati ya track yangu ''playa haters'' au nyimbo yangu nyingine ambayo iko tayali ''Sinyorita''
Nachowahimiza wasanii wa Tanzania kama wanataka kwenda next level...haina budi kufanya video na JanB Multimedia pamoja na director wangu Duncan Mukada...Bei zetu sio ghali sana na hatubabaishi. Director wangu keshafanya kazi na wasanii wakubwa sana hapa Sweden ,Marekani na anafanya video quality yeyote ile inategemea na budget ya msanii, pia tunafanya na TV commercial katika makampuni, documentally n.k
Kwa habari zaidi wapenzi wangu wa muziki na maendeleo ya Tanzania watembee site yangu ya kizalendo katika kutangaza muziki na uzuri wa Tanzania bure www.janbonline.com.

No comments:
Post a Comment