Thursday, June 14, 2012

Hii remix ya Hold Yah ya Stanboi katisha aiseee!



Muda mfupi uliopita kupitia Twitter msanii wa Tanzania aishie Wichita, Kansas, Marekani Stanboi amesambaza remix yake ya wimbo maarufu sana wa Gyptian Hold Yah!

Ni wimbo mfupi sana haufiki hata dakika mbili lakini ukiuskiliza utatamani kama ukikutana naye umwambie aungeze uwe na hata dakika nne hivi.

Kama angeiitoa remix hii kipindi ambacho wimbo original ulikuwa hot tunaamini ungemfikisha mbali sana hasa kama angeusambaza sehemu kubwa.

Kwa wale waliokuwa na doubt naye huenda wakimsikiliza humu wanaweza kubadilisha mawazo yao.

Well done Stanboi aka The African Child

No comments:

Post a Comment