Monday, June 4, 2012

Google Chrome yaipita Internet Explorer kama browser inayotumika zaidi


Chrome
Browser ya Google Chrome ilichukua nafasi ya pili nyuma ya Firefox kipindi kilichopita. Na sasa kwa mujibu ripoti ya  StatCounter, Chrome imeipiku Internet Explorer na kuwa browser inayotumika zaidi duniani.
Internet Explorer
Mabadiliko hayo yametokea kuanzia mwezi uliopita.

Mpaka sasa Google Chrome inashikilia market share ya asilimia 32.43, wakati Internet Explorer ikiwa na ya 32.12.

Firefox imekamata nafasi ya tatu ikiwa na share ya asilimia 25.55.

Firefox
Matumizi ya Internet Explorer yamekuwa yakipungua kwa kasi miaka ya hivi karibuni.

Safari
Browser ya computer za Apple, Safari nayo inapumulia mashine kwa kuwa na share ya asilimia 7.09 huku Opera ikiwa mwishoni kwa share ya asilimia 1.77.

Opera

No comments:

Post a Comment