Saturday, June 9, 2012
Don Jazzy atweet namba za vocha kibao, usharp wako tu
Katika kuhakikisha kuwa jina lake na la label yake mpya ya Mavin Records inakuwa karibu zaidi na mashabiki, jana producer Don Jazzy ameamua kugawa voucher kibao.
Producer huyo ambaye jina lake ni Michael Collins ametweet namba za vocha za mitandao yote ya simu nchini Nigeria.
Kwa haraka haraka ametoa vocha zinazoweza kufikia thamani ya shilingi laki mbili hivi.
Anachofanya ni kuzitweet namba hizo na yule ambaye ataziona haraka na kuziingiza kwenye simu yake basi ndo atakuwa amepata vocha kirahisi hivyo.
“Thank you very much My great Don & Nigeria's № 1 producer for the voucher, I'm dancing *Azonto* #1500 unit No Joke o.” ametweet mmoja wa mashabiki walioziwahi credits hizo za bure.
Katika hatua nyingine jana Don Jazzy ameonesha kuwa licha ya kuvunjika kwa label yake na ‘D’Banj, Mo’Hits, bado wana mawasiliano mazuri kwa kumpongeza kwa kuzaliwa leo, “SHOUT OUT TO THE GREATEST ENTERTAINER OUT OF AFRICA @IAMDBANJ HAPPY BIRTHDAY BRO. HAVE ALL THE FUN IN THE WORLD. GOD BLESS.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment